Tuesday, December 23, 2014

FEDHA ZA TEGETA ESCROW NI ZA IPTL-JK.




Rais Jakaya Kikwete leo amezungumza na taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam ambapo alitoa ufafanuzi kuhusu sakata la akaunti ya escrow ya Tegeta, huku akisisitiza kuwa fedha hizo ni za IPTL bali si za umma kama ilivyopotoshwa na wanasiasa wengi.

Ifuataya ni mazungumzo yake moja kwa moja kuhusu sakata hilo; "Wakati wa bunge la bajeti kulitokea madai kuwa fedha za escrow zilizokuwa benki kuu zimechotwa kinyemela na PAP kwa kushirikiana na viongozi wa serikali. Serikali iliahidi kutekeleza kwa kupitia kwa CAG kufanya ukaguzi ambayo ilisomwa bungeni pia niliagiza kuchapishwa kwenye magazeti na tovuti ya serikali,
TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi wao, taarifa yao ni kuwaona mahakamani, hawana ya maelezo. Tarehe 8 Desemba nilipoanza kazi, niliyasoma na kutoa maagizo, zipo taarifa nilizozipata japo sio zote, lakini nilisema siwezi kusubiri sana. Katika kusoma makaratasi na kupewa maelekezo, yapo mambo manne mikataba ya umeme, umiliki wa PAP, kodi ya serikali na tuhuma za rushwa.

Mikataba ya kununua umeme unaozalishwa na makampuni binafsi, mikataba ya umeme iko ya namna mbili tozo ya umeme ikiwa ni malipo ya umeme uliotumiwa kulingana na bei waliyokubaliana na ya pili ni gharama ya uwekezaji(capacty charge) kwa Songas, Aggreko, IPTL

Anaelezea historia ya mgogoro wa TANESCO na IPTL, TANESCO na IPTL walikubaliana kuanzisha akaunti ya Tegeta escrow benki kuu na kuingia mkataba, wizara ya madini kwa niaba ya TANESCO na IPTL na benki kuu kama wakala. Masharti ilikua kampuni ya IPTL itaendelea kupeleka madai yake TANESCO ya tozo ya uwekezaji na TANESCO itaendelea kulipa lakini yataenda escrow akaunti badala ya IPTL lakini ya umeme yaliendelea kwenda IPTL na ilifunguliwa 2006 na mpaka kesi kuamuliwa 2013 wakati IPTL inachukuliwa na PAP walikua hawajamalizana. (They decided to manage the crisis rather than resolve it)

Kwa mujibu wa mkataba, TANESCO isipolipa inatozwa riba ya 2%, kwa mujibu wa taarifa akaunti ilikua na 202.9 bilioni na sio 309.7, hizi zilipaswa kuwepo endapo TANESCO ingelipa zote kwa wakati.

Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL
Nianze kuelezea ya Escrow ni kitu gani, ni tofauti kidogo na akauti zetu tatu tulizozizoea, na akauti maalumu na kazi maalumu pia ikiisha na yenyewe inafungwa, inasimamia na wakala na wakala pia anajukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.

Akaunti ikafunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka tozo ya uwekezaji, zinahifadhiwa ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao lakini kabla ya hapo TANESCO walikua wanalipa moja kwa moja.

Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, mdhibiti wa hesabu alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL, Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikua wanalipa moja kwa moja lakini baada ya mzozo walikubaliana kwanza waziweke BoT.
Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya TANESCO yakakubali ya tozo kupunguzwa, kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za TANESCO ambazo lazima zirudi kwa kiasi kilichopunguzwa. Bahati mbaya miaka saba baadae halikuwa limefanyika.

Kama katika fedha hizo ipo kodi ya serikali, kwa mujibu kulikua na kodi ya ongezeko la thamani ambayo haikulipwa, IPTL hawakuilipa na uthamini ulikua bilioni 21 na ushee, TRA imepeleka madai yake kwa PAP.

CAG aliwaelekeza TANESCO kuacha kuhesabu pesa walizolipa kwenye akaunti ya escrow kama pesa zao, pesa hazikufikia sifa kuhesabika kama mali ya TANESCO(Asset). Mahakama kuu ya Tanzania ilifanya uamuzi katika shauri la maombi ya VIP, kusimamisha mchakato wa ufilisi wa IPTL na mahakama ikakubali.




0 Responses to “FEDHA ZA TEGETA ESCROW NI ZA IPTL-JK.”

Post a Comment

More to Read