Tuesday, December 23, 2014
RAIS MUGABE ATIMUA MAWAZIRI
Do you like this story?
Raisi wa
Zimbabwe Robert Mugabe amewafukuza kazi mawaziri wake wawilina manaibu waziri
wapatao watano hatua ambayo imemkumba aliyekuwa makamu wake Joyce Mujuru.
Hatua hii ya kuwafuta kazi mawaziri wake inafuatia
hali tetet ya kisiasa nchini humo na kujiandaa na lolote litakalo tokea lakini
pia ni kutokana na mafanikio hafifu ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka
tisini endapo atajiuzulu ama kufa.
Mugambe ambaye siku za hivi karibuni ameamua kupumzika
katika msimu huu wa sikuku na kuchagua bara la Asia kupumzika yeye na familia
yake.lakini wadadisi wa mambo wanasema mafanikio ya Raisi huyo ambayo ni hafifu
hayakutarajiwa na walio wengi.
Hofu ya kupokwa madaraka aliyonayo Rais Mugabe
ilimsukuma kumtimua kazi makamu raisi wake bi Jopyce Mujuru aliyekuwa akipata
umaarufu mkubwa kisiasa nchini mwake , na ndipo mkewe bi Grace Mugabe ambaye
naye amepanda umaarufu kisiasa na hivyo kumtia Joyce kumshauri afanye hivyo.
Mujuru aliingia katika kashfa ya kutaka kumuua
raisi,lakini pia anashutumiwa kukigawa chama cha ZANUPF,na linguine kuonekana
kushindwa kwa Mujuru kufunga mikataba ya kibiashara
Kufuatia tuhuma hizo nafasi ya bi Mujuru ilichukuliwa
na waziri Emerson Mnangwaga mshirika wa miaka mingi wa raisi Mugabe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS MUGABE ATIMUA MAWAZIRI”
Post a Comment