Tuesday, December 23, 2014
MADEREVA MBEYA WAFIKIWA NA HUDUMA YA ''WAIT TO SEND''
Do you like this story?
Kampeni ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia
sheria za usalama barabarani iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya
Ndani,Mheshimiwa Mathias Chikawe,leo imeendelea mjini Mbeya.
Madereva wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha
tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya
Butusyo Mwambelo amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya
ajali “Watumiaji wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi
kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate
matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema
Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa
ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga hususani katika kipindi hiki
cha msimu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya na aliipongeza kampuni ya Vodacom
kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo
limekuwa sugu.
Kwa upande wake,Mkuu wa kanda ya Nyanda za juu wa Vodacom Tanzania
Macfadyne Minja, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali kuunga
mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la
ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunaomba
madereva kufuata sheria za barabarani kwa usalama wenu,usalama wa abiria
mnaowabeba na watumiaji wengine wa barabara".
Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za
kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni ya
"Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria
za usalama barabarani.Mbali na kampeni hii alisema kwa mwaka huu kampuni
ilidhamini Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.
Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika
uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es
Salaam,Mwanza,Arusha na kampeni itaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini
Katika kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa
usalama barabarani na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabani walitoa
uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo vya moto
na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu
za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva
kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa
wanaendeshwa vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MADEREVA MBEYA WAFIKIWA NA HUDUMA YA ''WAIT TO SEND'' ”
Post a Comment