Thursday, December 18, 2014
MAHAKAMA YATOA AMRI WATU WAVAE KONDOMU WAKIENDA KUANGALIA SINEMA
Do you like this story?
Kwa nchi nyingi za
Afrika hasa Tanzania zinapiga marufuku kubwa ya uonyeshwaji wa movie za ngono
kutokana na kwamba hazina maadili mazuri kwenye jamii, ukienda nchi kama China
wao wameenda mbali zaidi, sheria kali zimewekwa ili kuzuia kabisa mtu yeyote
kucheza filamu hizo, ama kuuza.
Nchi za Ulaya na
Marekani zimekuwa zikishutumiwa kuruhusu biashara zote, kutengeneza na kuuza
movie hizo, lakini hii kutoka Los Angeles, Marekani imeweka sheria
inayowalazimu waigizaji wa filamu hizo za ngono kuvaa mipira maalum ya
kuwakinga na maambukizi ya magonjwa, Condom.
Sheria hii ambayo
ilianza kama muswada mwaka 2012 inawalazimu waandaaji wa filamu hizi pia
kulipia ada maalum ili kupewa kibali cha kufanyia kazi hiyo.
Waandaaji wengi wa
filamu za ngono wamelalamikia sheria hii wakidai kuwa inakwenda kinyume na haki
zao za msingi japo Mahakama imetoa tayari msimamo wake.
Wadau wa industry ya
filamu hizo wamedai kuwa wanafahamu fika hatari zilizoko kwenye maambukizi
na wanachukua hatua za kupunguza maambukizi haya kwa kuwakinga na kuwapima watu
wote wanaoshiriki uigizaji wa filamu hizi kabla ya kuingia nao mikataba ambapo
utaratibu huu mpya unawapa hofu waandaaji hao kwamba huenda soko la biashara
yao likayumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAHAKAMA YATOA AMRI WATU WAVAE KONDOMU WAKIENDA KUANGALIA SINEMA ”
Post a Comment