Friday, December 19, 2014
WALIOPITA JKT WAWAHIWA NA POLISI KABLA YA KUANDAMANA JIJINI DAR
Do you like this story?
Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu jijini Dar es Salaam limezuia maandamano ya
vijana waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kuwataka Kuteua
viongozi watano kwenda Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kuwakilisha malalamiko
yao.
Vijana haa ni waliopitia operesheni Mkapa, Utandawazi, Jiajili, Miaka 40, Kasi mpya, Maisha bora, Uadilifu pamoja na Kilimo kwanza toka mwaka 2000 hadi 2014.
Vijana hao zaidi ya 300 walianza maandamano hayo saa mbili asubuhi kutoka Jangwani kuelekea Ikulu wakiwa wamebeba bendera zenye rangi nyekundu na vyeti walivyohitima mafunzo yao na walipofika eneo la Hospitali ya Ocean Road, polisi walizuia maandamano hayo na kuwataka kuchagua viongozi watakao wawakilisha.
Askari hao waliwataka wengine kuondoka eneo hilo na kutafuta eneo lenye usalama kwenda kuwasubiri viongozi wao watakapotoka Ikulu na kuwaletea majibu.
Mmoja wa kiongozi wa mafunzo, Magesa Maijo, alisema lengo la maandamano yao ni kupeleka kilio chao kwa Rais kutokana na kutopewa majibu sahihi kwa wizara husika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WALIOPITA JKT WAWAHIWA NA POLISI KABLA YA KUANDAMANA JIJINI DAR ”
Post a Comment