Friday, December 19, 2014
WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015 WATAJWA.
Do you like this story?
Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). |
Jumla ya wanafunzi
438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliohiyimu elimu ya msingi mwaka huu
wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani.
Idadi hiyo ni sawa an
asilimia 97 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.
Taarifa ya Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa waandishi wa
habari leo imesema ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na
mwaka jana.
Hata hivyo, jumla ya
wanafunzi 12, 432 waliofaulu, hawajapata nafasi ya kuchaguliwa kuendelea na
masomo ay sekondari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uungufu wa majengi,
hali inayowalazimisha kusubiri chaguo la pili litakalofanyika mapema mwakani.
Jumla ya wanafunzi
808,085 walisajiliwa kufanya mtihani wa taifa mwaka 2014 lakini ni wanafunzi
792,122 tu ndio waliofanya mtihani, hiyo ikiwa ni asilimia 98.02% ya
wanafunzi wote waliosajiliwa.
Taarifa ya Tamisemi
inaongeza kuwa wavulana wanaongoza kwa kuchagaliwa zaidi ya wasichana ambapo
jumla ya wavulana 219,964 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hiyo
ikiwa ni sawa na asilimia 97.28 ya wanafunzi wote waliochaguliwa huku wasichana
wakifikia 218,996 ambayo ni sawa asilimia 97.1 ya wanafunzi waliochaguliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015 WATAJWA.”
Post a Comment