Friday, December 19, 2014
LIGI YA SOKA SOMALIA KUTIMUA VUMBI LEO.
Do you like this story?
Sasa tunaelekea Somalia ambako
wakati mwingi habari zinazosikika ni ghasia, ukame na mifarakano miongoni mwa
koo. Lakini sasa tunapata habari nzuri. Baadaye leo, ligi ya kandanda nchini
humo inatarajiwa kutimua vumbi. Mashindano ya mwaka huu yatashuhudia idadi
kubwa ya wachezaji wa kigeni.
Kuongezeka kwa hali ya utulivu
katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kumevutia kiasi cha wachezaji ishirini wa
soka kutoka Nigeria, Kenya, Uganda na nchi nyingine za Kiafrika.
Pia kuna kocha wa kigeni. Ni
John Maura ambaye anakuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuongoza klabu kubwa nchini
Somalia kwa karibu miaka thelathini. Ameingia mkataba wa mwaka mmoja kufundisha
timu ya Banadir Sports Club, ambao ni mabingwa wa ligi ya Somalia.
Timu kumi zitakuwa zikiwania
ubingwa mwaka huu, zikiwa zimeongezeka timu mbili kutoka nane za mwaka jana.
Kwa mji mkuu Mogadishu kuwa na
kipindi kirefu cha utulivu katika zaidi ya miongo miwili, Mamlaka ya michezo
nchini humo wnataka askari wa Umoja wa Afrika, AMISOM, nchini humo kuondoka
katika uwanja wa mpira, eneo ambalo ni kubwa kuliko yote ya michezo nchini
Somalia, ili michezo ianze kufanyika katika uwanja huo.
Lakini majeshi ya Amisom,
ambayo yamekuwa katika uwanja huo tangu mwaka 2011, wakati kundi la wapiganaji
wa Kiislam la al-Shabaab liliporudishwa nyuma, bado majeshi ya Amisom
hayajaondoka katika uwanja huo.
Badala yake uwanja wa Banadir,
uliofanyiwa matengenezo na shirikisho la soka duniani, FIFA mwaka jana,
utatumika kwa michezo ya mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “LIGI YA SOKA SOMALIA KUTIMUA VUMBI LEO.”
Post a Comment