Friday, December 19, 2014
BALOTELLI AFUNGIWA MCHEZO MMOJA NA FAINI
Do you like this story?
Chama cha Soka nchini Uingereza, kimemfungia mchezo mmoja,
mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli ikiwa ni adhabu kutokana na kile
Super Mario alichokiandika katika mitandao ya habari ya kijamii.
Adhabu
hiyo itamlazimisha nyota huyo wa Italia, kukosa mchezo wakati timu yake ya
Liverpool itakapoikaribisha Arsenal Jumapili, katika michezo ya ligi kuu ya
England. Pia amepigwa faini ya pauni£25,000 na lazima ahudhurie kozi ya elimu.
Baloteli
mwenye umri wa miaka 24 ameadhibiwa kwa mujibu wa sheria za FA kwa kutuma
ujumbe ambao umeonekana kuwa na ubaguzi.
Balotelli
amekubali adhabu hiyo lakini ameiandikia FA ili iweze kumpunguzia.
Baada
ya kujua adhabu yake, aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook kwamba
uamuzi wa FA "umeonyesha wazi" kwamba ujumbe wake ulikuwa
"makosa".
Balotelli
aliituma picha iliyotolewa na mtu mwingine tofauti. Alisema: "nasikitika
kwamba wachezaji wenzangu na mashabiki wa Liverpool FC wataadhibiwa kwa kosa
ambalo nimelifanya na sasa najutia. Ni dhamira yangu kukubaliana na uamuzi wa
FA na kuhakikisha kuwa halitatokea tena."
Msemaji
wa Liverpool amesema: "klabu inatambua uamuzi uliofikiwa na jopo huru la
FA na utapewa uzito unaostahili mara tutakapoupokea kutoka FA.
"Hatua
yoyote itakayochukuliwa nasi kuhusiana na jambo hili itakuwa kati ya klabu na
mchezaji."
Mchezaji
huyo wa zamani wa Manchester City Balotelli alirudia kutuma picha ya mchezo wa
kompyuta yenye kibonzo cha Super Mario katika mtandao wa Instagram ambacho
kilikuwa na maneno "ruka kama mtu mweusi na kusanya sarafu kama
myahudi."
Baadaye
alituma ujumbe wa tweeter akikanusha kuwa ujumbe huo ulikuwa na makosa, kabla
ya kuomba radhi.
Balotelli
alirejea katika kikosi cha Liverpool kilichocheza na Manchester United katika
uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya kukosa michezo sita kutokana na
maumivu ya nyama za paja. Katika mchezo huo Liverpool iliambulia kipigo cha
magoli 3-0.
Balotelli
ameifungia magoli mawili timu yake katika mechi 15 alizoichezea timu ya
Liverpool tangu atoke AC Milan msimu uliopita wa kiangazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BALOTELLI AFUNGIWA MCHEZO MMOJA NA FAINI”
Post a Comment