Friday, December 19, 2014

ANGALIA VIDEO JINSI WABUNGE WALIVYOCHAPANA MAKONDE HUKO KENYA


Kikao cha Bunge la Kenya kilisimama kwa takribani dakika 30 kutokana na kutofautiana kwa Wabunge hao kuhusiana na msimamo wao kutofautiana wakati wakiendelea na mjadala unaohusu mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Nchi hiyo kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye masuala ya Usalama.

Wabunge wa upinzani walipinga muswada huo kwa kutupa karatasi chini, Bunge likaahirishwa ambapo hali ya hewa ilikuwa mbaya na baadaye Wabunge hao kupigana, wengine wakichaniana nguo na hata kuumizana.
Wabunge wa Upinzani waligomea muswada huo na kuanza kuimba, Bunge hilo likasitishwa.

Nimekurekodia sauti wakati habari hiyo ikiripotiwa na kituo cha WBS unaweza kubonyeza play kuisikiliza, pia kuna video kutoka K24 ambayo unaweza kuitazama hapa.


0 Responses to “ANGALIA VIDEO JINSI WABUNGE WALIVYOCHAPANA MAKONDE HUKO KENYA ”

Post a Comment

More to Read