Monday, December 22, 2014
WANAUME 28 WASHTAKIWA KWA UASHERATI
Do you like this story?
Wanaume 28 wameshtakiwa kwa kufanya uashertai nchini Misri. |
Watu 28 wamefikishwa mahakamani mjini Cairo Misri
kutokana na mashtaka ya uasherati katika kile kinachoonekana kama ishara za
kampeni dhidi ya ushoga.
Baadhi ya washtakiwa walikuwa wakilia baada ya
kufikishwa mahakamani wakiwa wamefungwa pingu.
Mmoja alilalama kwamba yeye na wafungwa wenzake
walipigwa na polisi.
Wanaume hao walikamatwa mapema mwezi huu katika
kidimbwi cha kuoga kwa jina hammam mjini Cairo.
Wanahabari wa chombo kimoja cha habari walichukua
filamu ya uvamizi huo wa polisi.
Miezi miwili iliopita,watu wanane walifungwa miaka 3
jela baada ya kunaswa katika kanda ya video ambayo wakuu wa mashtaka wanasema
ilionyesha wakifanya harusi ya watu wa jinsia moja mjini Cairo.CHANZO BBC
SWAHILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAUME 28 WASHTAKIWA KWA UASHERATI”
Post a Comment