Monday, March 2, 2015
NEC YAONGEZA MUDA WA KUJIANDIKISHA MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE.
Do you like this story?
Waziri mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda
ameahidi kuigawa wilaya ya Chunya ili kupata wilaya mbili kabla ya uchaguzi
mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Uamuzi wa waziri mkuu kuigawa wilaya ya
Chunya haraka unatokana na maombi ya wananchi wa jimbo la Songwe hususan katika
kijiji cha Buyuni ambao wameamua kulala chini kwenye mavumbi, huku mbunge wa
jimbo la Songwe, Mheshimiwa Philip Mulugo akipiga magoti chini na kumwomba
waziri mkuu kuigawa wilaya hiyo kwa madai kuwa ina maeneo makubwa kijiografia
hali ambayo inakwamisha maendeleo ya wananchi.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya akamweleza waziri
mkuu kuwa ukubwa wa wilaya ya Chunya ni asilimia 46 ya ardhi yote ya mkoa wa
Mbeya hivyo maombi ya wananchi hao yana hoja ya msingi, huku wa wilaya ya
Chunya Deodatus Kinawiro akielezea uwezo wa halmashauri ya wialaya ya Chunya
kiuchumi kuwa inajitegemea kwa asilimia 15.
Waziri mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda
amesema kuwa kikwazo pekee cha kuigawa wilaya hiyo ni idadi ndogo ya watu,
lakini kutokana na hali ambayo ameiona analazimika kuigawa wilaya hiyo haraka,
jambo ambalo ameahidi kulifanya kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NEC YAONGEZA MUDA WA KUJIANDIKISHA MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE.”
Post a Comment