Thursday, October 15, 2015
JANUARY MAKAMBA APANGUA KOMBORA LILILORUSHWA WIZARANI MWAKE
Do you like this story?
SERIKALI imeeleza kushangazwa na uzushi kwamba siku ya
uchaguzi mkuu, data za mawasiliano pamoja na umeme vitazimwa, jambo ambalo
imetaka wananchi kupuuza taarifa hizo potofu.
Taarifa hizo ambazo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba ameziita ni uzushi, zinadaiwa kutolewa na baadhi ya
wanasiasa wa vyama vya upinzani wakidai kwamba serikali imepanga kufanya hivyo
ili wananchi washindwe kupata taarifa za matokeo ya uchaguzi.
“Kwanza napenda ifahamike kuwa hakuna chama chochote cha
siasa kitakachofaidika kikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM), endapo data za
mawasiliano zitazimwa, hivyo nawaomba wananchi wasiamini maneno ya uzushi
yasiyo na ukweli hata chembe,” alisisitiza
January.
Alisema huduma ya data zina umuhimu mkubwa katika uchumi wa
Tanzania kuliko siasa, kwani kwani ofisi nyingi zikiwemo taasisi za kibenki
zinategemea data hizo katika shughuli zake za kila siku.
“Sasa ukisema tutazima data ni sawa na ku-paralyze
(kusimamisha) uchumi kwani watu hawataweza hata kutoa fedha zao benki, jambo
ambalo ki ukweli haliwezi kufanyika,” alisisitiza.
Alisema ni Wizara yake na Serikali kwa ujumla, imekuwa
ikilinda na kurekebisha mitandao kuhakikisha inafanya kazi vizuri hasa katika
kipindi hicho cha uchaguzi kutokana na ukweli kuwa kutakuwa na taarifa nyingi
zinazohitajika kufikia wananchi.
“Hatutegemei watu kutumia vibaya mitandao ya kijamii na
kusababisha taharuki lakini hata wakifanya hivyo, Sheria ya kudhibiti mitandao
ipo, itatumika kudhibiti na si kuzima data kama inavyodaiwa,” alisema
January.
Aidha alisema taarifa hizo zilizosambazwa ambazo hata yeye
ameziona, zinasambazwa na wanasiasa wenye nia ya kutengeneza hamaki kwa
wananchi jambo ambalo si sahihi.
Wakati huo huo, msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Adrian Severine, alisema kwa sasa shirika hilo, haliwezi kuzungumzia jambo hilo, hadi pale wanasiasa wote wanaodai mtaani kuwa wanazo taarifa za kuzimwa umeme nchini siku ya uchaguzi watoe uthibitisho.
Wakati huo huo, msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Adrian Severine, alisema kwa sasa shirika hilo, haliwezi kuzungumzia jambo hilo, hadi pale wanasiasa wote wanaodai mtaani kuwa wanazo taarifa za kuzimwa umeme nchini siku ya uchaguzi watoe uthibitisho.
“Huu ni wakati wa uchaguzi, hawa wanasiasa watasema mengi
tu, sasa sisi kama shirika hatuwezi kusema lolote wala kukanusha taarifa hizi
mpaka hao wanaodai kuwa wana taarifa kuwa tumeamriwa tuzime umeme
watuthibitishie. Siwezi kukanusha kitu ambacho hakina uthibitisho,” alisisitiza Severine.
Alisema kwa sasa shirika hilo, limeamua watu wote
watakaozusha taarifa kuhusu utendaji au shughuli za shirika hilo na kuthibitika
kuwa ni uongo, wataburuzwa mahakamani ili iwe fundisho. “Kuna watu
tayari tumewafungulia mashitaka kwa ama kuandika au kuzungumzia taarifa za
uongo kuhusu Tanesco, kesi zinaendelea mahakamani,” alisema.
Juzi katika mkutano wa viongozi wa siasa ulioandaliwa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari, alidai
kuwa chama hicho kinazo taarifa za uhakika kuwa siku ya uchaguzi umeme na data
vitazimwa ili wananchi washindwe kupata taarifa za uchaguzi. Pamoja na kiongozi
huyo, kutoa kauli hiyo, pia baadhi ya mitandao nayo imekuwa ikisambaza taarifa
hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JANUARY MAKAMBA APANGUA KOMBORA LILILORUSHWA WIZARANI MWAKE”
Post a Comment