Friday, October 23, 2015

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TAMWA YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI


Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini wakiwa Jijini Mbeya  katika Semina ya siku tatu juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.

Mwezeshaji wa mafunzo toka Tamwa, Jamilah
Abdallah akionyesha mfano wa Gazeti kwa Waandishi wa Habari Jinsi ya kuandika Habari katika kipindi hiki cha uchaguzi  kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Nyanda
za juu kusini kuhusu kuandika habari zenye lengo la kuwashirikisha
wanawake kushiriki zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu
unaotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)



Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini wakiwa Jijini Mbeya  katika Semina ya siku tatu juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)

Majadiliano yakiendelea(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini wakiwa Jijini Mbeya  katika Semina ya siku tatu juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.




Fredy Jackson kutoka Mbeya Fm Radio akionyesha moja kati ya  Gazeti ambalo alikuwa na Habari yoyote inayomuhusu mwanamke.

Fredrick Mabula kutoka Kings Fm Njombe akisoma moja ya habari ambayo ilikuwa na uchochezi.




Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini wakiwa Jijini Mbeya  katika Semina ya siku tatu juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.




NA SAMWEL NDONI MBEYA,
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zitakazosaidia
jamii kuondokana na dhana ya kuwadharau wanawake kuwa hawezi kufanya
kitu chochote kwenye jamii.

Aidha wametakiwa kujikita kuandika habari zitakazotoa fursa kwa wanawake kushiriki kwenye uchaguzi ili wapate nafasi ya  kuwawakilisha watu kwani wao wana uwezo sawa na wanaume.

Hayo yamesemwa  na Mwezeshaji wa mafunzo toka Tamwa, Jamilah
Abdallah wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Nyanda
za juu kusini kuhusu kuandika habari zenye lengo la kuwashirikisha
wanawake kushiriki zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu
unaotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika Jijini Mbeya kwa kuwashirikisha
waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe
,Rukwa,Ruvuma.

Alisema kwamba waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuhakikisha
wanawake wanashiriki kikamilifu kwenye zoezi la kupiga kura, kuomba au
kupigiwa kura.

Hata hivyo Mwezeshaji huyo alisema kuwa kwenye jamii nyingi nchini
wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kuzuiwa kushiriki
kugombea au kupiga kura kutokana na imani potofu zilizojengeka
miongoni mwa jamii kuwa hawawezi kuwaongoza wanaume jambo ambalo
linawanyima fursa kuwawakilisha wananachi.

Aidha, Jamilah aliwataka kufanya tathmini za ahadi zinazotolewa na
wagombea kwa kuhoji mikakati itakayotekeleza ahadi hizo ili kumjenga
kisaikolojia mwananchi kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua kiongozi
atakayewaletea maendeleo.


Aliwakumbusha kuzingatia miiko na maadili ya taaluma yao wakati huu wa
kuelekea uchaguzi mkuu ili ufanyike kwa haki na amani.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa wajibu wa
mwandishi katika kipindi hiki ni kuzifahamu sera za vyama vya siasa
ili waweze kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ikiwa ni pamoja na
kuhamasisha amani.

‘’Mwandishi wa habari ili aweze kufanya kazi yake vizuri katika
kipindi hiki hana budi kuzisoma na kuelewa sera za vyama vya siasa ili
awaelimishe wananchi kuhusu sera hizo na utekelezaji wake’’ alisema
Fredy Jackos (Mbeya)

Mwandishi mwingine Paulina Kuye kutoka Iringa alisema ‘’Ni vizuri
waandishi wa habari katika kipindi hiki tujikite kuhamasisha wagombea
kuhubiri amani pindi wanapokuwa jukwaani, pamoja na kuandika habari za
makundi maalum yanayosahaulika mara kwa mara wakiwemo wazee, walemavu

na wanawake’’alisema.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanaendeshwa na Chama cha waandishi wa
habari wanawake kwa kushirikiana na Shirika la kihabari la
kimataifa(Internews).

Lengo la mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ni jinsi ya kuandika
habari za uchaguzi kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na namna ya kuweza
kuisaidia jamii kuelewa dhima zima ya uchaguzi wa amani na utulivu.

0 Responses to “ KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, TAMWA YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI”

Post a Comment

More to Read