Monday, October 26, 2015

MATOKEO YA UCHAGUZI KATA MBALIMBALI ZA WILAYA YA MAKETE




Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Luwumbu wilaya ya Makete mkoani Njombe usiku huu wa saa 06:01 amemtangaza mgombea udiwani wa CCM kuwa ni mshindi wa kata hiyo katika uchaguzi uliofanyika jana

Msimamizi huyo Bw Barton Mbedule amemtaja Mgombea wa CCM Bw Enock Ngajilo kuwa ameibuka mshindi kwa kupata kura 588 dhidi ya mgombea wa CHADEMA aliyepata kura 284
hapa chini ni matokeo ya udiwani tu
Kata ya Ipelele, Alimivu Sanga wa CCM amepata kura 882 na Mwipelele Mbogela amepata kura 1,074, hivyo kutangazwa mshindi

Kata ya Bulongwa mgombea wa CHADEMA amepata kura 595 na Benayo Luvanda wa CCM amepata kura 793


kata ya Kipagalo Reuben Mwandilava wa CCM amepata kura 765 Alfred Nsemwa wa CHADEMA amepata kura 643


Kata ya Iwawa Baton Sanga ACT-Wazalendo amepata kura 39, Ona Nkwama wa CCM amepata kura 2,107 Asifiwe Luvanda wa CHADEMA amepata kura 2,206 na ndio aliyeibuka Mshindi


Katika kata ya Isapulano Dadiso Tweve ACT - Wazalendo amepata kura 277, Aginiwe Mahenge wa CCM amepata kura 406, na Alphonce Mbilinyi wa CHADEMA amepata kura 485


Kata ya Ukwama mgombea wa CHADEMA Vasco Chaula amepata kura 330, na mgombea wa CCM Augustino Luota amepata kura 947


Kata ya Iniho mgombea wa CHADEMA amepata kura 437 na mgombea wa CCM Jison Mbalizi amepata kura 958


Kata ya Mang'oto mgombea wa CHADEMA amepata kura 224 na mgombea wa CCM Othmund Idawa ameibuka mshindi kwa kupata kura 923


nyingine zinakuja, endelea kutufuatilia

0 Responses to “ MATOKEO YA UCHAGUZI KATA MBALIMBALI ZA WILAYA YA MAKETE”

Post a Comment

More to Read