Wednesday, November 4, 2015

WANANCHI WAFANYA UHARIBIFU KATIKA BARABARA YENYE KIWANGO CHA KIMATAIFA JIJINI MBEYA


Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mbeya Mhandisi Paul Lyakurwa akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya  ya Mbeya  Nyilembe Munasa jinsi wananchi wanavyokata alama za barabara ya kwenda chunya.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) 


Mkuu wa Wilaya  ya Mbeya  Nyilembe Munasa akiongea na wananchi wa isanga(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mbeya Mhandisi Paul Lyakurwa akitoa maelezo kwa wananchi wa Iganzo juu ya umuhimu wa alama za barabarani

Moja kati ya Alama iliyokatawa na wananchi.







Siku chache mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara Mbeya –Chunya yenye kilomita 72 ambayo inafadhiliwa na serikali kwa asilimia 100 kumeibuka kwa wizi wa miundombinu ya barabara hiyo .

Baadhi ya miundo mbinu iliyoibiwa katika barabara hiyo ni pamoja na alama za kuongozea magari (road signs) pamoja na reli zilizowekwa kwenye kingo za barabra .

Akizungumza  na wananchi   waishio kando ya barabara ya mbeya –chunya Mkuu wa Wilaya  ya Mbeya  Nyilembe Munasa amesema mradi wa sehemu ya kwanza  Mbeya –Lwanjilo  kilomita 36 ambao unatekelezwa na makandarasi wa China communications construction  company(CCCo) limited kwa gharama ya shilingi bilioni 55 umeanza kuhujumiwa na watu wasio fahamika.

Amesema jumla ya alama 43 za barabarani na reli zenye urefu wa mita 4 zimeibiwa katika kipindi cha mwezi octobar mwaka huu ambazo  thamani yake  shilingi milioni 6 .
Kufuatia hatua hiyo Mkuu huyo wa wilaya ametoa wito kwa wananchi waishio pembezoni mwa barabara hiyo ambao ni Isanga,Iganzo ,Mwansekwa na Ilowelo kuhakikisha wanakuwa walinzi na watunzaji wa thamani zilizopo katika barabara hiyo.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi hao  kutofanya shughuli za kilimo katika eneo la hifadhi ya barabara ambalo ni mita 30 kutoka katika barabara kila upande kama ilivyo ainishwa kwenye sheria ya barabara Na 13 ya 2007.

Kwa upande wake amesema kitendo kilichofanywa na watu hao ni aibu kubwa kwani mkoa mzima wa mbeya barabara hiyo ndio pekee ilikuwa na alama zenye viwango vya kimataifa hivyo hatuanhiyo imerudisha nyuma maendeleo ya mkoa.
Mwisho.

1 Responses to “WANANCHI WAFANYA UHARIBIFU KATIKA BARABARA YENYE KIWANGO CHA KIMATAIFA JIJINI MBEYA”

Unknown said...
November 5, 2015 at 10:37 AM

Isanga bhana,maendeleo ya kwetu wenyewe halafu mijitu inaibuka na kuibaaa miundo mbinu..........shame on us.


Post a Comment

More to Read