Wednesday, December 16, 2015
JENISTA ATOA SIKU 14 KUKAGUA MIKATABA YA AJIRA
Do you like this story?
![]() |
| Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. |
Dar es Salaam.
Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa siku 14 kwa maofisa kazi wote nchini, kukagua
mikataba ya ajira kama inaendana na kanuni na sheria za ajira nchini.
Mhagama alitoa agizo hilo jana jijini Dar es
Salaam, alipotembelea kiwanda cha kutengeneza nguo cha Tooku Tanzania Germent
kilichopo Mabibo External, ambacho wafanyakazi wake waligoma Jumatatu ya wiki
hii wakiomba kuongezwa mishahara .
Akiwa ameongozana na Naibu wake, Antony
Mavunde, na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage aliwataka
maofisa kazi kumpa mrejesho baada ya siku 14, huku akitaka uongozi wa kiwanda
hicho kumpa majibu ya malalamiko ya wafanyakazi hao ndani ya saa nane.
“Jambo hili halikubaliki wakati kuna maofisa
kazi wameajiriwa kwa ajili ya kazi hii. “Naomba mnipe maelezo ya kutosha baada
ya siku hizo 14 na uongozi wa kiwanda hiki, nawapa saa nane hadi kufika saa
10:00 jioni(jana) muwe mmenipa majibu sahihi kama mtawaongezea mishahara au
mnafunga kiwanda,” alisema.
Awali, Mhagama alikutana na wafanyakazi wa
kiwanda hicho na kuwataka kuendelea na shughuli zao wakati wakitafuta ufumbuzi
wa kudumu wa tatizo hilo.
“Waziri ametuomba tuendelee na kazi suala
letu litatatuliwa, tumekubali kuendelea na kazi tukisubiri majibu ya waziri na
uongozi ili tujue mwisho wetu nini,” alisema Faith Ruben mmoja wa wafanyakazi
kiwandani hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ JENISTA ATOA SIKU 14 KUKAGUA MIKATABA YA AJIRA”
Post a Comment