Wednesday, December 16, 2015
SIMBACHAWENE AKUNJUA MAKUCHA AAGIZA TAKATAKA ZOTE ZIZOLEWE KABLA YA DESEMBA 20
Do you like this story?
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala
bora George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na
wakurungenzi wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote
zilizokusanywa wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu.
Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na
wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya Tamisemi
mjini Dodoma.
Alisema kuwa hataki kuona hadi ifikapo tarehe 20 ya mwezi
huu kuwa uchafu wa siku ya uhuru bado unaendelea kulalamikiwa na watu kuwa bado
haijaondolewa katika maeneo uliokusanywa.
“Hadi ifikapo tarehe hiyo sitaki kusikia uchafu bado
haujaondolewa katika maeneo ulipokusanywa toka siku ya uhuru lakini pia
unapoondolewa huo kuna uchafu mwingine unakuja hivyo basi watendaji wanaohusika
wa hakikishe kuwa wanaanda maeneo ya kuupeleka” alisema Simbachawene.
Aidha aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika
utendaji wa kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani awamu ya tano ya
haitaendelea kuwalea watendaji wavivu.
Kwa upande wake,Naibu Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo,
aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wao wa zamani ili
waweze kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “ SIMBACHAWENE AKUNJUA MAKUCHA AAGIZA TAKATAKA ZOTE ZIZOLEWE KABLA YA DESEMBA 20”
Post a Comment