Tuesday, December 8, 2015
WAFANYA BIASHARA MBEYA WAJITOLEA ZANA ZA USAFI KWAJILI YA 9 DISEMBA
Do you like this story?
Viongozi wa Idara Mbalimbali wakiwa wameshika vifaa Mbalimbali vya Usafi. |
Vifaa Vya Usafi |
Afisa Habari wa Almashauri ya jiji la Mbeya Bi Jackline Msuya (Kulia)akiwa na wakuu wa Idara ya Usafirishaji wakati wa upokeaji wa Vifaa vya Usafi.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Katika kuelekea
siku ya kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika ya zamani au Tanzania Bara ya sasa
ambayo imeamriwa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa siku ya
kufanya usafi kwa Tanifa zima, wafanya biashara wa eneo la Kabwe hapa Jijini
Mbeya wameungana na kutoa msaada wa vitendea kazi ili kurahisisha kazi ya siku
hiyo.
Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya nyenzo hizo ambazo ni
Toroli 1,koleo 12, leki 10,mifagio 20,Gam buti 5,maski 30 na Grofsi 20 na kwa
upande wa msemaji wa wafanya biashara hao Makamu Mwenyekiti wa maduka ya Stendi
ya Kabwe bw. Emmanuel Ndaki amesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano huo wa kutoa
Vifaa Mbalimbali kwani wanatambua kuwa Usafi ni wa watu wote kwa ujumla
Pamoja na hayo afisa habari wa halmashauri ya
jiji la Mbeya, Jack Msuya amesema kwamba maandalizi yanakwenda vizuri kuelekea
siku hiyo ya tarehe 9 disemba na kusema kwamba kazi ya usafi sasa kwa jiji la
Mbeya itakuwa ya muendelezo na sio zima moto kama watu wadhanivyo.
Amesema kwamba halmashauri ya jiji la Mbeya
sasa imejidhatiti kutunza hali ya usafi katika mitaa ya jiji na hata kuweka
sheria kwa wachafuzi wa mazingira ambapo sasa akikutwa mtu anachafua mazingira
atatozwa kiasi cha Tsh. 50,000 kama adhabu.
Pamoja na hayo afisa habari huyo kwa niaba ya
mkurugenzi wa jiji la Mbeya amewashukuru wafanya biashara hao kwa msaada wao wa
vifaa vya usafi lakini akatoa wito pia kwa watu wengine walio na uwezo wa
kujitolea vitendea kazi kufanya hivyo ili kurafisisha zoezi la kulifanya jiji
la Mbeya kuwa safi.
Agizo la sikukuu ya Uhuru ambayo hufanyika
tarehe 9 disemba ya kila mwaka kuwa siku ya usafi lilitolewa na rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, mhe. Dkt John Pombe Magufuli siku chache baada ya
kuapishwa kuwa rais wa chini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
katika maeneo mbalimbali ya nchi kutokana na kukithiri kwa uchafu katika
mazingira yanayowazunguka wananchi.
Kwa Habari na Matukio Mbalimbali endelea kutembelea www.faharinews.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAFANYA BIASHARA MBEYA WAJITOLEA ZANA ZA USAFI KWAJILI YA 9 DISEMBA ”
Post a Comment