Friday, January 29, 2016
MALINZI: TUMEKOSEA KUIRUHUSU AZAM
Do you like this story?
Said Ally, Dar es Salaam
KUFUATIA malalamiko ya klabu kadhaa za Ligi Kuu Bara juu ya Azam FC kuruhusiwa kwenda nchini Zambia wakati ligi hiyo ikiendelea, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeibuka na kuomba radhi juu ya kitendo hicho.
KUFUATIA malalamiko ya klabu kadhaa za Ligi Kuu Bara juu ya Azam FC kuruhusiwa kwenda nchini Zambia wakati ligi hiyo ikiendelea, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeibuka na kuomba radhi juu ya kitendo hicho.
TFF iliipa ruhusa Azam kwenda Zambia
kushiriki michuano maalumu iliyoandaliwa na timu ya Zesco ya nchini humo ambapo
kikosi hicho kiliondoka Jumatatu ya wiki hii na kusababisha michezo yao miwili
kupigwa kalenda, hali ambayo imezua taharuki miongoni mwa timu za ligi kuu
ambazo nazo zimekuja juu na kutaka zipewe ruhusa ya kusafiri.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi, jana alizungumza
na wanahabari na kusema kuwa wanaziomba radhi timu za ligi kuu kwa kitendo
kilichotokea cha kuipa ruhusa Azam kwa kuwa hakikuwa katika utaratibu mzuri.
“Kiukweli tunaomba radhi kwa kitendo ambacho
tumekifanya kwa kuipa Azam ruhusa ya kwenda Zambia hali ambayo imezua taharuki
kwa timu nyingine na kusababisha wao pia kuomba ruksa ya kwenda nchi
mbalimbali, lakini tutajitahidi kuwabana pale watakaporudi kwa kuwachezesha
mara mbili kwa wiki ili kuwafanya wawe sawa kimichezo na wenzao.
“Lakini niseme tu kuwa tumekosea kwa Azam
lakini hatutaki kuona timu nyingine zinachukulia mwanya huo nao kuleta barua
zao kwa kutaka kwenda nje ya nchi kama ilivyofanyika kwa timu hiyo.
“Hatutakuwa tayari kufanya jambo ambalo
tumelikosea na tunasema hatutaipa ruhusa timu yoyote ile hata hawa Yanga ambao
nimesikia wanaomba kwenda Afrika Kusini safari hiyo haitakuwepo, watambue
hilo,” alisema Malinzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MALINZI: TUMEKOSEA KUIRUHUSU AZAM”
Post a Comment