Wednesday, January 13, 2016
NAIBU WAZIRI WA FEDHA DKT ASHATU KIJAJI AIAGIZA TRA MBEYA KUKUSANYA MAPATO KWA WABADILISHAJI WA FEDHA TUNDUMA
Do you like this story?
Naibu Waziri Fedha na Mipango
Dkt,Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya (
hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara katika Mpaka wa Tunduma na
Zambia
|
ameitaka
Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa
ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamili kwa biashara ya
ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.
Naibu waziri
huyo ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato
(TRA) Mkoani humo na kutoa tathimini ya ziara yake aliyoifanya
katika Mpaka wa Tunduma na Zambia.
Amesema
serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara
hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo ameitaka mamlaka
hiyo kuhakikisha inaweka mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato
yake kutokana na biashara hiyo.
Amesema
serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjali na
kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa
kodi.
Amebainisha
kuwa nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi
na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu.
Sehemu nyingine
ambayo ameiagiza mamlaka hiyo kuishughulikia mara moja ili serikali iweze
kupata mapato yake ni pamoja kuibuka kwa Saccos pamoja vikundi mbalimbali
ambavyo vimekuwa vikijihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa liba kubwa hali
ambayo pia imekuwa ikiwapa mzigo mkubwa wananchi .
Katika hatua
nyingine Naibu waziri huyo ameuagiza uongozi wa mamlaka ya mapato (TRA)
Katika mpaka wa Tunduma na Zambia kuhakikisha kuwa mizigo yote inayosafilishwa
kupitia mpaka huo inafanyiwa tathimini na kulipiwa kwa muda wa usio zidi siku
moja tayari kuendelea na safari kwa inayoingia na kutoka nje ya Tanzania.
Ziara
ya Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza Mkoani Mbeya tangu alipoteuliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika
wadhifa huo.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NAIBU WAZIRI WA FEDHA DKT ASHATU KIJAJI AIAGIZA TRA MBEYA KUKUSANYA MAPATO KWA WABADILISHAJI WA FEDHA TUNDUMA ”
Post a Comment