Friday, March 4, 2016

BARCELONA YAVUNJA RECODI YA REAL MADRID ILIYOWEKWA MSIMU WA 1888/1889




Mabingwa wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Barcelona usiku wa kuamkia Ijumaa wamefanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa na wapinzani wao wakubwa, Real Madrid baada ya kupata ushindi wa goli tano kwa moja walpokuwa wakipamabana na Rayo Vallecano.

Barcelona wamevunja rekodi ya kucheza michezo 35 bila kufungwa na kuipita rekodi ambayo Madrid waliiweka ya kucheza michezo 34 bila kufungwa msimu wa 1888/1889 ambapo ni miaka 27 iliyopita.

Mchezaji bora wa mchezo huo alikuwa ni Lionel Messi abaye alifunga hat trick katika dakika ya 23, 53 na 72, magoli mengine yalifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 22 na Arda Turan dakika ya 86 huku goli la kufutia machozi la Rayo Vallecano likifungwa na Contreiras Gonçalves.

Aidha Rayo Vallecano ilimaliza mchezo huo ikiwa nusu baada ya wachezaji wake wawili Diego Llorente  dakika ya 42 na Manuel Iturra dakika ya 67 kuonyeshwa kadi nyekundu.

Baada ya matokeo hayo, Barcelona imefikisha alama 69 ikiwa katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi hiyo ikifuatiwa na Atletico Madrid iliyo na alama 61, Rayo Vallecano wao wameshuka nafasi moja kutoka ya 16 hadi 17 na ikiwa na alama 26.

0 Responses to “ BARCELONA YAVUNJA RECODI YA REAL MADRID ILIYOWEKWA MSIMU WA 1888/1889”

Post a Comment

More to Read