Thursday, March 3, 2016
MKAPA KUWA MSULUHISHI WA MGOGORO WA BURUNDI.
Do you like this story?
Rais wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa, ameteuliwa kuwa msuluhishi wa
mgogoro unaoendelea kuikumba nchi ya Burundi kwa muda unaokaribia mwaka mmoja
tangu April 2015.
Mkapa ameteuliwa kuwa msulıuhishi wa mgogoro
wa huo na marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika
mkutano uliofanyika jana Jumatano, mjini Arusha.
Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa EAC, Dkt. John Pombe Magufuli aliyasema
haya katika mkutano huo mjini Arusha
na kuongeza kuwa Benjamin Mkapa ameteuliwa ili kumsaidia rais wa Uganda, Yoweri
Museveni kutatua mgogoro wa Burundi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MKAPA KUWA MSULUHISHI WA MGOGORO WA BURUNDI.”
Post a Comment