Wednesday, March 2, 2016

KERR AMKINGIA KIFUA ISIHAKA.




Omary Mdose, Dar es Salaam
BAADA ya nahodha msaidizi wa Simba, Hassan Isihaka kusimamishwa na uongozi wa klabu hiyo kwa kile kilichoelezwa ni utovu wa nidhamu, aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Muingereza, Dylan Kerr amesema haamini kama kweli mchezaji huyo amefanya kosa kama hilo.

Juzi Jumatatu Simba kupitia kwa Haji Manara ambaye ni Mkuu wa Idara ya Habari klabuni hapo, ilitangaza kumsimamisha Isihaka kwa siku zisizojulikana kwa kosa la kumtolea maneno yasiyokuwa na staha kocha wake, Jackson Mayanja kabla ya mchezo wao wa Jumapili iliyopita wa Kombe la FA dhidi ya Singida United.

Mbali na kusimamishwa huko, pia Kamati ya Utendaji ya Simba imeagiza Isihaka kulipwa nusu mshahara kwa kipindi chote cha adhabu yake hiyo.

“Isihaka ni mchezaji mzuri na mwenye nidhamu, hivyo sidhani kama kweli anaweza kufanya kitendo kama hicho kwani kwa muda niliokaa naye sikuwahi kuona akiwa mtovu wa nidhamu.

“Lakini Mayanja anapaswa kuelewa kwamba amepata bahati sana kurithi mikoba yangu pale Simba, hawezi kukaa vizuri na wachezaji kwani hata alipokuwa Coastal wachezaji walikuwa wakimlalamikia, sidhani kama atakuwa na maisha marefu pale,” alisema Kerr.

0 Responses to “ KERR AMKINGIA KIFUA ISIHAKA.”

Post a Comment

More to Read