Wednesday, March 2, 2016
MFANYAKAZI WA NDANI AMCHINJA MTOTO WA MIAKA 4
Do you like this story?
Picha za CCTV zinaonesha mwanamke huyo aliyevalia hijab akitembea nje ya kituo cha usafiri akiwa amebeba kichwa cha mtoto. |
Polisi huko
Moscow wamemkamata mwanamke baada ya kupatikana amebeba kichwa cha mtoto.
Kanda ya video
inamuonesha mwanamke huyo akitembea karibu na kituo cha basi akiwa amebeba
kichwa hicho mikononi.
Alikamatwa na
polisi na kupelekwa kufanyiwa uchunguzi wa akili.
Mwanamke huyo
Gyulchekhra Bobokulova, kutoka jamhuri ya Uzbekistan anatuhumiwa kwa kumuua
mtoto huyo msichana kabla ya kuchoma moto nyumba ya wazazi wake.
Picha za CCTV
zinaonesha mwanamke huyo aliyevalia hijab akitembea nje ya kituo cha usafiri
akiwa amebeba kichwa cha mtoto.
Afisa mmoja wa
ulinzi anaonekana akimkabili na kumbwaga sakafuni kabla ya kumfunga pingu.
Bi Bobokulova
amekamatwa na sasa anafanyiwa uchunguzi wa kiakili kubaini iwapo ana uwezo wa
kubaini vitendo vyake.
Taarifa kutoka
kwa afisi ya upelelezi wa jinai mjini Moscow inasema ’’ maafisa wameanzisha
shughuli ya kubaini chanzo cha kifo cha mtoto ambaye kiwiliwili chake
kilipatikana katika kitongoji cha Narodnoye Opolcheniye Magharibi mwa Moscow’’.
"'Uchunguzi
wa awali unaonesha kuwa yaya aliyekabidhiwa jukumu la kumtunza mtoto huyo
mwenye umri kati ya miaka 3-4 alisubiri hadi wazazi wake na kakake mkubwa
wakaondoka kabla ya kumuua na kisha kuchoma moto nyumba yao’’.
''Chanzo cha
tukio hilo kwa hakika hakijabainika ila tumemkamata yaya huyo ambaye alizaliwa
mwaka wa 1977 katika jamhuri ya Uzbekistan,'' taarifa hiyo iliongezea.
Afisa mwengine
wa polisi ambaye hakutaka kutajwa anasema kuwa ''mtoto huyo alichinjwa na
kiwiliwili chake kikachomwa moto.
Kichwa chake
hakikupatikana kwenye eneo la tukio.''
Kwa mujibu wa
jarida la kirusi la Life News, mwanamke huyo aliulizwa na askari polisi wa
kituo cha usafiri cha Oktyabrskoye Polye, kitambulisho chake.
Hapo
ndipo alipogutuka na kutoa kichwa cha mtoto huyo kutoka kwenye mkoba wake na
kusema kwa sauti ya juu kuwa yeye ni gaidi na kuwa alikuwa malaika wa kifo na
kuwa angejilipua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MFANYAKAZI WA NDANI AMCHINJA MTOTO WA MIAKA 4 ”
Post a Comment