Wednesday, March 2, 2016

MAFUTA YASHUKA BEI, ZIPO HAPA BEI MPYA.




Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za mafuta ya aina ya Petroli, Mafuta ya Taa na Diseli.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugrnzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi amesema mafuta ya Petroli yamepungua kwa shilingi 31, Dizeli imepungua kwa shilingi 114 na Mafuta ya Taa kwa shilingi 234.

Ngamlagosi alisema bei mpya zinaanza kutumika leo Machi, 2 sasa Dar es Salaam mafuta ya Petroli itauzwa 1,811, Dizeli 1,486 na Mafuta ya Taa 1,465.

Aidha alisema kuwa bei kwa mkoa wa Tanga haitapungua kutokana na bandari ya mkoa huo kutokupokea mafuta mapya katika bandari hiyo na hivyo wataendelea kutumia bei za mwezi Februari.

0 Responses to “ MAFUTA YASHUKA BEI, ZIPO HAPA BEI MPYA.”

Post a Comment

More to Read