Monday, March 7, 2016
MAHAKAMA SINGIDA YAWAHUKUMU MAJANGILI SABA KWENDA JELA MIAKA 140 NA FAINI YA BILIONI 1.9
Do you like this story?
Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Singida, imewahukumu majangili saba adhabu
ya kutumikia jela ya miaka 140 na kulipa faini ya zaidi ya shilingi 1.9 bilioni
baada ya kuwatia hatiani kwa kwa makosa 12 likiemo la kumiliki bunduki ya
kijeshi SMG waliyokuwa wanaitumia kuulia Tembo.
Baadhi ya makosa mengine ni kuunda umoja /ushirikiano wa kufanya uhalifu
wa kuuawa wanyapori wakiwemo Tembo, kufanya biashara haramu ya
kuuza nyara za serikali na kumiliki meno ya Tembo bila kwa na kibali.
Washitakiwa hao ambao kesi yao ilipewa namba 5/2015, ni Yusuph Masala
Jidavi (39) mkulima kijiji cha Yongo Manda mkoani Katavi, Elias John
Sprian (30) mkazi wa Kijiji cha Ng’ambe mkoani Tabora na Salum Mohammed Ngasa
(31) mkazi wa kijiji cha Imalampaka Sasilo wilaya ya Manyoni.
Wengine ni Yona Stanley @Yohana (26) mkazi wa kijiji cha Mbwasa
Sasilo wilaya ya Manyoni, Ramadhani Salum Hatibu (33) mkulima kijiji cha Mgulu
wa Ng’ambe wilaya ya Manyoni,Kulwa Saidi Salum (28) mkulima kijiji cha Sikonge
mkoani Tabora na Buhoro Salehe Lubaha Yakonie (37)@ Buhoro mkazi wa
Kambi ya Wakimbizi Katumba mkoani Tabora.
Mwendesha mashtaka na mwanasheria wa serikali Pretrida Mutta, alidai mbele
ya Hakimu mfawidhi mwandamizi na mahakama hiyo, Joyce Minde, kuwa kati ya
Agosti mwaka 2013 na Julai nane mwaka 2014, washitakiwa kwa pamoja walikamatwa
wakimiliki vipande 28 vya meno ya Tembo vyenye thamani zaidi ya shilling 34.1
milioni.
Mutta alisema pia washitakiwa hao walikamatwa wakimiliki kinyume na
sheria ‘Elephant tufts’ sita zenye thamani ya shilingi 192 milioni, kipande cha
ngozi ya Simba chenye thamani ya zaidi ya shilingi 7.8 milioni na ngozi ya kudu
ya shilingi 3.5 milioni.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu, Mwanasheria wa serikali Mutta, aliiomba
mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washitakiwa, ili iwe fundisho kwao na
kuogofya watu wengine wanaotarajia kujihusisha biashara haramu ya kuuza nyara
za serikali.
Kwa upande wa washitakiwa ambao wakili wao na kujitegemea Josephat Wawa
ambaye hakuwepo Mahakamani, washitakiwa kila mmoja kwa wakati wake, aliiomba
mahaka hiyo impe adhabu nafuu kwa madai mbalimbali likiwemola kutegemewa na
familia.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Minde, alisema kuwa upande wa mashitaka
umethibitisha bila kuacha chembe chembe ya shaka kwa hali hiyo washitakiwa wana
hatia kama walivyoshitakiwa.
“Kila mshitakiwa atatumikia jela miaka 20 na kulipa faini ya zaidi ya
shilingi 274.2 milioni adhabu hizi ni fundisho kwenu na pia kuwaogofya watu
wengine wanaotarajia kutenda makosa ya aina hii”,alisema Hakimu Minde.
Imeandaliwa na Na Nathaniel Limu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAHAKAMA SINGIDA YAWAHUKUMU MAJANGILI SABA KWENDA JELA MIAKA 140 NA FAINI YA BILIONI 1.9 ”
Post a Comment