Sunday, March 6, 2016

MANCHESTER UNITED WAPIGWA KIDUDE NA WEST BROM






Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) leo imeendelea leo kwa michezo miwili, mchezo wa kwanza ukiwa ni Crystal Palace iliyokuwa wenyeji wa Liverpool na wapili ulikuwa West Bromwich waliokuwa nyumbani kuwakabili Manchester United.

Mchezo wa Liverpool ulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2 – 1, Magoli ya Liverpool yakifungwa na Roberto Firmino dk. 72 na Christian Benteke dakika ya 90+4 na goli la Crystal likifungwa na Joe Ledley dakika ya 49.

Mchezo wa pili wa Manchester United umemalizika kwa wenyeji West Brom kuifunga Mnchester United goli moja kwa bila, goli lililofungwa na José Rondon katika dakika ya 67.

Baada ya matokeo ya michezo ya leo, Liverpool imefikisha alama 44 ikiwa nafasi ya saba, Manchester United imesalia na alama 47 ikiwa nafasi ya sita, West Brom imefikisha alama 39 na kushika nafasi ya 11 na Crystal Palace ikiwa na alama 33 na kuwa nafasi ya 15 ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

0 Responses to “MANCHESTER UNITED WAPIGWA KIDUDE NA WEST BROM ”

Post a Comment

More to Read