Wednesday, March 9, 2016

SERIKALI YAWAPA MOTISHA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA WANAWAKE" TWIGA STARS"


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (wapili kushoto) akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wachezaji wa Twiga Stars jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi  na kutoka kulia ni Meneja Masoko wa TFF Peter Simon na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA) Bi. Amina Karuma.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA) Bi. Amina Karuma (katikati) akielezea jambo wakati wa mkutano baina ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (kushoto) na wachezaji wa Twiga Stars (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo wachezaji walihakikishiwa kupokea ahadi yao kama walivyo ahaidi kwa kuwa wamefanikiwa kuifunga timu ya Taifa wanawake Zimbabwe licha ya kutoibuka na ushindi. Kulia ni Meneja Masoko wa TFF Peter Simon. (Picha zote na Frank Shija, WHUSM)

Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo wachezaji walihakikishiwa kupokea ahadi yao kama walivyo ahaidi kwa kuwa wamefanikiwa kuifunga timu ya Taifa wanawake Zimbabwe licha ya kutoibuka na ushindi.


Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetimiza ahadi yake ya kuwapa motisha wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” kwa kuwapa kila mmoja shilingi Laki tatu taslimu kutokana na kufanikiwa kutikisa nyavu za Zimbabwe licha kutoibuka na ushindi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia James Wambura wakati wa mkutano wake na wachezaji hao jijini Dar es Salaam.

Wambura alisema pamoja na Twiga Stars kufungwa kwa magoli 2-1 bado mmejitahidi sana katika ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwenye mashindano kama hayo walikuwa wanafungwa hadi magoli matano kwa sifuri.

Aliongeza kuwa kutokana na jitihada hizo anatimiza ahadi yake ya kumpatia kila mchezaji kiasi cha shilingi 300,000/= fedha ambazo anaamini zitawazidishia hari na morali ya ushindi katika mchezo wa marudiano.

“Kutoka na na jitihada zenu mlizozionyesha wakati wa mchezo huo ninatoa kwa kila mchezaji kiasi cha shilingi 300,000/=  na ahadi hii inaendelea tena katika mchezo wa marudiiano” Alisema Naibu Waziri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA) Amina Karuma alitoa wito kwa wachezaji kuhakikisha katika mechi ya marudio wanashinda kwa hari na mali ili kuonyesha thamani umuhimu wao
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuendelea kujitokeza kusaidia maendeleo ya michezo hasa Soka la wanawake kwani kumekuwa na changamoto ya wafadhili hali inayopelekea kusuasua.

Motisha hiyo kwa wachezaji imetokana na michango ya wadau mbalimbali awalioguswa na timu hiyo wadau waliochangia mpaka sasa ni TCRA (10,000,000/=), ASAS(2,000,000/=), Mohamed Enterprises (2,000,000/=) na mdau ambaye akupenda jina lake litajwe (3,000,000/=) na kufanya mpaka sasa kuwa na jumla ya shilingi milioni 17. 

Kwa wadau wanaopenda kuchangia watumie Akaunti namba 20110001677 Twiga Stars Special Fund NMB Bank House, kwa wale wanaotaka kuchangia vifaa waiwasilishe Wizarani mtaa wa Ohio Jengo la Golden Jubilee Ghorofa ya nane.
Imetumwa na Frank Shija, WHUSM

0 Responses to “SERIKALI YAWAPA MOTISHA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA WANAWAKE" TWIGA STARS"”

Post a Comment

More to Read