Saturday, March 5, 2016
SUMATRA KUWAPELEKA MAHAKAMANI MADEREVA NA MAKONDA.
Do you like this story?
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi Usafiri wa Majini na Nchi
Kavu (SUMATRA), Mkoa wa Kilimanjaro kuwafikisha mahakamani
madereva wote na makondakta wanaowatoza abiria nauli kubwa tofauti na
zilizopangwa na ofisi hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Afisa Mfawidhi Bw.Tadei Mwita alipokuwa
akijibu kero ya mkazi wa mkoa huo kwa njia ya simu iliyotolewa na
Gazeti la Mwananchi Machi 04, mwaka
huu,iliyozungumzia daladala zinazofanya safari zake kati ya Moshi
Mjini – Himo kuwatoza nauli ya shillingi 1000 abiria wanaoshuka maeneo ya
Kiboriloni, Sango Pumuani na Kawawa road tofauti na nauli iliyopangwa na
SUMATRA katika vituo hivyo.
“Kuanzia wiki ijayo wadau wote watakao kuja kuomba leseni kwa
ajili ya usafirishaji wa abiria ndani ya mkoa huu watahitajika kuonyesha nauli
watakazo toza abiria katika vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho
cha safari zao,” alisema Bw.Mwita.
Bw.Mwita alisema hivi sasa SUMATRA Mkoa wa
Kilimanjaro imeanzisha utaratibu wa kuwataka wadau wote wanaotarajia
kuanza kutoa huduma za usafiri wa daladala mkoani hapo kuonyesha nauli watakazo
toza katika vituo vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho.
Hata hivyo Afisa huyo aliwashauri wakazi wa maeneo kama
kiboriloni kwa sasa kupanda daladala za Kiboriloni kwa kuwa zipo nyingi ili
kuepuka usumbufu unaojitokeza.
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SUMATRA KUWAPELEKA MAHAKAMANI MADEREVA NA MAKONDA.”
Post a Comment