Sunday, March 13, 2016
ZIARA YA SIKU MBILI YA NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI MKOANI MBEYA.
Do you like this story?
Mwonekano wa Guba ( Dampo) lililopo Nsalaga jijini Mbeya |
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Dt. Samweli Lazaro akitoa ufafanuzi wa Ujengwaji wa Dampo hilo la kisasa kwa Naibu waziri wa Tamisemi Mhe. Suleiman Jaffo.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mwonekano wa Machinjio Mpya ya N"gombe ambayo yataanza kutumika hivi karibuni yaliopo katika Wilaya Mpya ya songwe Eneo la Utengule. |
Naibu waziri wa Tamisemi Mhe. Suleiman Jaffo alifanya Ziara katika Hospitali ya Mkoa jijini Mbeya kujionea utendaji wa kazi na changamoto Mbalimbali. |
Naibu waziri wa Tamisemi Mhe. Suleiman Jaffo akiangalia Barabara za mradi wa Benki kuu ya dunia. |
Naibu
waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mhe. Suleiman Jaffo
yuko jijini Mbeya katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili ambapo katika siku
yake ya kwanza amefanya ziara katika hospitali ya mkoa wa Mbeya, Shule ya
sekondari ya Iyinga Tech pamoja na guba (dampo) la kisasa la jijini Mbeya na
mradi wa barabara za benki kuu ya dunia.
Katika
ziara hiyo naibu waziri, mh. Jaffo alianzia katika shule ya sekondari ya Iyunga
Tech ambayo hivi karibuni imekumbwa na majanga mawili ya moto mfululizo na
kusababisha hasara kuaffobwa za mali za wanafunzi na shule hiyo.
Mhe.
Jaffo ametoa pole baada ya kutokea majanga hayo ya moto katika shule ya Iyunga
Tech na kuahidi kusimamia ukarabati wote wa shule hiyo mpaka itakapokuwa katika
hali ya kawaida huku akipongeza jitihada
zinazofanywa ili kulifanyia kazi agizo lake la kukarabatiwa mapema shule hiyo
ili ifikapo tarehe mosi mwezi ujao wa Aprili wanafunzi watakaporejea shuleni
wakute mazingira mazuri ya kusomea.
Pamoja
na hayo mhe. Jaffo ametoa agizo kwa hospitali ya mkoa wa Mbeya kuhakikisha
wanapata kiwanja kilichopo karibu na hospitali hiyo ili ijengwe mara moja
hospitali maalumu ya wakina mama wenye matatizo mbalimbali, pia amepongeza utendaji
kazi wa hospitali hiyo na na kutatua changamoto zilizo chini ya watendaji wa
hospitali hiyo ya mkoa wa Mbeya.
Aidha
mhe. Jaffo ametembelea mradi uliokamilika wa guba la kisasa ambalo litahudumia
wakazi wote wa halmashauri ya jiji la Mbeya.
Ziara
ya naibu waziri wa TAMISEMI mhe. Suleiman Jaffo anaendelea na ziara leo ikiwa
ni siku ya pili ya ziara hiyo hapa mkoani Mbeya ambapo atatembelea soko jipya
la Mwanjerwa na baadae jioni atazungumza na wafanyakazi wote wa mkoa wa Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ZIARA YA SIKU MBILI YA NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI MKOANI MBEYA.”
Post a Comment