Thursday, April 28, 2016
SERIKALI KUWASILISHA MSWADA WA SHERIA YA NDOA.
Do you like this story?
Serikali
imejiandaa kuleta Muswada wa Sheria bungeni kutoa haki ya kusoma kwa
watoto wote wa kike na kiume wa shule za msingi, sekondari na kutoruhusiwa kuoa
au kuolewa.
Aidha,
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali inaendelea
kukamilisha utaratibu wa kupata maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya Sheria
ya Ndoa na kutungwa kwa Sheria mpya ya Mirathi na Urithi kuondokana na
mkanganyiko uliopo kuhusu sheria hiyo.
Bunge
lilielezwa hayo jana mjini Dodoma wakati waziri huyo akijibu swali la nyongeza
la Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene (CCM) aliyehoji ni lini serikali itaanza
maandalizi ya kuchukua maoni juu ya kufanya marekebisho sheria ya ndoa ya mwaka
1971.
Akijibu
swali hilo, Dk Mwakyembe alisema hatua za awali zimeshaanza kuchukuliwa na
wizara hiyo ili kupata maoni ya wananchi juu ya marekebisho ya sheria hiyo ya
ndoa ya mwaka 1971 na kutungwa kwa sheria mpya ya mirathi na urithi.
Alisema
serikali ina nia ya dhati ya kufanyia marekebisho sheria ya ndoa na kwamba
mchakato huo ulisitishwa kwa kuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba ilikuwa
ikikusanya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba , hivyo walidhani wananchi
wangetoa pia maoni juu ya sheria hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ SERIKALI KUWASILISHA MSWADA WA SHERIA YA NDOA.”
Post a Comment