Wednesday, August 24, 2016
JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA NDANI YA VYAMA VYA SIASA
Do you like this story?
Kutokana
na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini, leo
August 25 2016 Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano yote ya kivyama ndani
na nje ili kuzuia machafuko ya amani yanayoendelea kujitokeza katika kipindi
hiki.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es salaam Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP
Ernest Mangu amesema Jeshi la polisi halikuzuia mikutano ya ndani ya siasa
kwasababu lilikuwa linaamini ni mikutano iliyokuwa ikizungumzia maendeleo
ya wananchi
Amesema
Jeshi hilo limebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika kuchochea
wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya mapambano na jeshi
la polisi
"Kwasababu
hiyo basi,kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria
na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga
marufuku mikutano yote ya ndani" amesema
IGP Ernest Mangu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA NDANI YA VYAMA VYA SIASA”
Post a Comment