Sunday, September 11, 2016
DAKTARI ALIYEWAAMBUKIZA UKIMWI WAGONJWA 200 ATUPWA JELA MIAKA 25
Do you like this story?
Daktari aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini
Cambodia amehukumiwa jela.Daktari huyo bandia alipatikana na hatia ya
kuwaambukiza takriban watu 200 virusi vya ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo
cha miaka 25 jela kwa makosa yake.
Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia.
Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia.
Yem Chrin alikuwa akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji cha Roka bila ya kujua alickuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi.Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini upande wa mashtaka ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.
Kesi hiyo imefichua uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa
raia kupata huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.
Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.
Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “DAKTARI ALIYEWAAMBUKIZA UKIMWI WAGONJWA 200 ATUPWA JELA MIAKA 25”
Post a Comment