Thursday, September 15, 2016
MCHUNGAJI AKATISHA HOTUBA YA TRUMP YA KUMPINGA CLINTON
Do you like this story?
Mchungaji wa kanisa moja la watu
weusi katika jimbo la Michigan, Marekani amemkatisha Donald Trump akihutubu
alipoanza kumshutumu mpinzani wake Hillary Clinton.
Mchungaji Faith Green Timmons alimkatisha BwTrump alipomshutumu
mgombea huyo wa chama cha Democratic kuhusu mikataba ya kibiashara duniani.
"Bw Trump, nilikualika hapa uje kutushukuru kwa juhudi ambazo
tumefanya Flint, si kutoa hotuba ya kisiasa," amesema pasta huyo wa kanisa
la Bethel United Methodist.
"Aha, hilo ni jambo njema," amemjibu mgombea huyo wa
chama cha Republican huku akionekana kuanza kucheza na karatasi alizokuwa nazo
jukwaani.
Bw Trump ameendelea na kuzungumzia kwa kifupi kuhusu kutatua
matatizo ya maji safi Flint, lakini baadhi ya watu kwenye umati wakaanza
kumzomea.
Mwanamke mmoja amesema kwa sauti kwamba mfanyabiashara huyo tajiri
alitumia njia za kibaguzi katika majumba yake.
Mfanyabiashara huyo amejibu: "Haiwezekani, umekosea.
Singeweza kufanya hivyo."
Mchungaji huyo ameingia tena na kuwashutumu waliokuwa wanamzomea
Bw Trump na kusema: "Yeye ni mgeni katika kanisa langu na
mtamheshimu".
Bw Trump
mwishowe amelazimika kukatiza ghafla hotuba yake, ambayo imedumu kwa dakika
sita hivi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “MCHUNGAJI AKATISHA HOTUBA YA TRUMP YA KUMPINGA CLINTON”
Post a Comment