Friday, September 9, 2016
MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS WAPATA AJALI
Do you like this story?
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani ambaoTulikuwa unaelekea wilayani
tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais Mtwara umepata ajali na kusababisha
majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya Rufaa Ligula.
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji
cha Nanguruwe kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Majeruhi walioumia ni
dereva pamoja na wasaidizi wanne wa
makamu Rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba
wasaidizi wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi
wa habari wa Channel Ten, StarTv na Clouds Tv liliacha njia na nusura
kupinduka.
Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba
si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali
iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha
majeruhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS WAPATA AJALI ”
Post a Comment