Friday, September 9, 2016
KUELEKEA DERBY YA MANCHESTER, HIZI NI TAKWIMU ZA HEAD-TO-HEAD KATI YA MOURINHO NA GUARDIOLA.
Do you like this story?
Kesho
ndiyo kesho jijini Manchester ambapo mafahari wawili wa jiji hilo Manchester
United na Manchester City watakuwa wakikabiliana uso kwa uso mchezo utakaopigwa
katika Uwanja wa Old Trafford majira ya saa 8:30 mchana.
Huu
unaelezwa kuwa mchezo utakaokuwa na uhasama mkubwa kuwahi kutokea kutokana na
uwepo wa makocha wawili ambao pia ni mahasimu wakubwa Jose Mourinho na Pep
Guardiola.
Ikumbukwe
hawa ni watu waliowahi kufanya kazi kwa pamoja wakiwa Barcelona wakati huo
Mourinho akiwa kocha msaidizi wa Louis van Gaal na Pep akiwa mchezaji ambaye
alikuwa anaelekea mwishoni.
Wakakutana
tena kama mahasimu, Guardiola akiinoa Barcelona na Mourinho akiwa upande wa
Real Madrid, na hapa ndipo uhasama wao uliposhika kasi.
Walicheza
mechi nyingi zilitoa matokeo tofauti-tofauti, lakini Guardiola akiibuka kinara
zaidi.
Angalia
jedwali la takwimu zao hapa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)



0 Responses to “KUELEKEA DERBY YA MANCHESTER, HIZI NI TAKWIMU ZA HEAD-TO-HEAD KATI YA MOURINHO NA GUARDIOLA.”
Post a Comment