Thursday, September 1, 2016

RAIS WA BRAZIL ANG’OLEWA MADARAKANI NA WABUNGE



Rais wa Brazil ameondolewa madarakani kwa kura 61 zilizopigwa na wabunge za kuto kuwa na imani na Rais wao

Makamo wake Michel Temer ameapishwa kuwa Raisi mpya wa Brazil mpaka pale uchaguzi mwingine utakapo fanyika January 2019

Rais Mpya wa Brazil Michel Temer amesema nchi yake inaingia katika enzi mpya ya matumaini baada ya kuondoshwa madarakani kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff.

Akizungumza na taifa hilo kupitia Televisheni, Rais Temer ametoa wito wa kuungana pamoja na kusema kuwa kuondolewa madarakani kwa bibi Rousseff kumemaliza miezi kadhaa ya mashaka.

Rais huyo amekutwa na hatia ya udanganyifu wa bajeti ya nchi hiyo wakati wa kampeni zake za uchaguzi miaka miwili iliyopita.
 


0 Responses to “RAIS WA BRAZIL ANG’OLEWA MADARAKANI NA WABUNGE”

Post a Comment

More to Read