Friday, December 9, 2016
MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YA UFUNDI YA MTWARA YATEKETEA KWA MOTO
Do you like this story?
Bweni
la wasichana wa shule ya sekondari ya Mtwara ufundi iliyoko katika Manispaa ya
Mtwara Mikindani limeteketea kwa moto leo majira ya saa moja asubuhi.
Akizungumza katika eneo la tukio kamanda polisi Mkoani hapa Thobias Sedoyeka amesema kwamba majira ya saa moja katika shule ya sekondari ufundi kulitokea moto ambao ulianza kuwaka katika mabweni ya wasichana ambapo mpaka sasa chanzo hakijajulikana na kuongeza kuwa hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu na makadirio ya hasara ya thamani ya jengo na mali zilikuwemo bado haijajulikana.
Naye
mwalimu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Nanyalika amesema kwamba
alikuwepo eneo la tukio wakati bweni hilo la wasichana wa shule ya sekondari ya
ufundi linaanza kuteketea ambapo kwa upande wake hajui chanzo cha moto huo hali
ambayo imepelekea walimu ambao wanaishi ndani ya shule hiyo kuwa na hali ya
sintofahamu kwa kuhofia usalama wao.
kwa
upande wake mwalimu wa shule ya sekondari Sululu Sekondari iliyoko Mjini Masasi
ambae yupo shuleni hapo kwa ajili ya kusahihisha mitihani ya kidato cha pili na
alikuwa akitumia moja ya chumba cha bweni hilo amesema kwamba kipindi ambacho
wapo katika maeneo yao ya kazi ndipo walipoona moshi unatokea kwenye bweni.
Naye
mwalimu Masele Francis kutokea shule ya sekondari ya Namwombe iliyoko katika
Halmashauri ya Masasi ameeleza kuwa kipindi ambacho anatoka bwenini aliona
moshi mkubwa hali ambayo ilimpelekea kurudi ndani ili kuwapa wenzake taarifa.
Aidha
Afisa Habari wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi.Jamad Omary amewatoa hofu
walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo na kuwaomba kuwa wavumilivu katika
kipindi hiki kigumu mbali na hayo amewataka wananchi wa Manispaa ya Mtwara
Mikindani kuwa na ushirikiano wa kutosha pindi kunapotokea tatizo kama hilo na
si kuishia kutoa lawama.
Hata
hivyo Kamanda amesema kwamba taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo ikiwemo
chanzo cha moto huo itatolewa baada ya taratibu zote kukamilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YA UFUNDI YA MTWARA YATEKETEA KWA MOTO”
Post a Comment