Friday, January 6, 2017

RIYAD MAHREZ NDIE MCHEZAJI BORA AFRIKA KWA MWAKA 2016




Tarehe 5, January 2017 jiji la Abuja nchini Nigeria ndio ilifanyika hafla ya utolewaji wa tuzo za soka za mwaka 2016 na shirikisho la soka barani Afrika CAF, hizi ni tuzo ambazo hutolewa kwa wachezaji waliyofanya vizuri kwa mwaka mzima kwa kupigiwa kura. Jana ndio ilikuwa hitimisho la kinyang’anyiro hichi ambapo mchezaji wa timu ya Taifa ya Algeria na timu ya Leicester City ya England Riyad Mahrez alitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika.

Mahrez alishinda tuzo hiyo baada ya kupata jumla ya kura 361, huku Pierre-Emerick Aubameyang akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 313 wakati Sadio Mane wa Liverpool amemaliza nafasi ya tatu kwa kupata kura 186.
Mwaka jana ulikuwa mwaka mzuri kwa Kijana Mbwana Samatta baada ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya Ndani, safari hii tuzo hii imekwenda tena kwa Afrika Mashariki na kutua katika nchi ya Uganda kwa Golikipa Denis Onyango  ambaye anacheza klabu ya Mamelodi Sundowns

Tuzo Nyingine zilikuwa kama ifuatavyo:

1.    Refarii bora wa mwaka imeenda kwa Bakary Papa Gassama


2.    Coach bora wa mwaka imekwenda kwa Pitso Mosimane anaiefundisha klabu ya Mamelodi Sundwons


3.    Timu Bora ya wanawake imekwenda kwa timu ya Taifa ya Nigeria
4.    Mchezaji Bora wa kike ni Asisat Oshoala


5.    Klabu bora ya Afrika imekwenda kwa Mamelodi Sundowns

6.    Timu bora ya Taifa imekwenda kwa timu ya taifa ya Uganda

0 Responses to “RIYAD MAHREZ NDIE MCHEZAJI BORA AFRIKA KWA MWAKA 2016”

Post a Comment

More to Read