Sunday, March 23, 2014

BABA MZAZI AUA MWANAYE KIKATILI KWA KIPIGO TUNDUMA...!!!


Kamanda wa polisi Mkoa Wa Mbeya Ahmed Msangi


Mtoto mwenye umri wa miaka saba, mjini Tunduma wilayani Momba, ameuawa kwa kushambuliwa kwa kipigo na baba yake mzazi akimtuhumu kwa uzururaji.

Irene Mbembela ambaye alikuwa akisoma shule ya awali, katika Shule ya Msingi Migombani, aliuawa juzi. 
 
Baba yake, Marko Mbembela (30) anayedaiwa kusababisha kifo hicho, inadaiwa alimwadhibu kwa kumchapa viboko sehemu mbalimbali za mwili wake hadi akapoteza fahamu.
 
Inadaiwa mtoto huyo alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Tunduma.
 
Hata hivyo, taarifa ya Kamanda Msangi iliyotolewa kwa vyombo vya habari, haikuelezwa kama baba huyo anashikiliwa na Polisi. 
 
Kamanda alitaka wazazi kutumia busara katika kuelekeza na kuonya watoto badala ya kuwapiga.

0 Responses to “BABA MZAZI AUA MWANAYE KIKATILI KWA KIPIGO TUNDUMA...!!!”

Post a Comment

More to Read