Monday, March 31, 2014
BUNGE LIVUNJWE TUKAWA OMBE RADHI WANANCHI MJUMBE.
Do you like this story?
Mivutano katika Bunge la Katiba imemchukiza
mmoja wa wajumbe wa chombo hicho, Michael Laizer ambaye amemshauri mwenyekiti
wake, Samuel Sitta amwombe Rais kuvunja Bunge.
Laizer pia amewataka wajumbe wenzake kurudi
katika maeneo yao ili wakaombe radhi kwa Watanzania kutokana na ufujaji wa
fedha unaotokana na kuwepo kwao kwenye vikao vya Bunge.
“Mwenyekiti narudia tena kama watu hawataki
uamuzi huu, nakushauri andika barua kwa Mheshimiwa Rais ili aje alivunje Bunge
na twende makwetu,” alisema Laizer.
Laizer alilishutumu Bunge hilo kuendelea
kutafuna fedha wakati watu wengine wanaishi maisha magumu zaidi kiasi cha
kushindwa kupata hata mlo mmoja kwa siku.
Alipinga muda ambao wametumia wajumbe hao kwa
ajili ya kujadili masuala ya kanuni pekee bila hata ya kufikia uamuzi, akisema
ndoto yake ni kuwa hadi wiki hii waanze kuchambua vifungu vya katiba.
Aidha amesema watu wenye umri mkubwa kama
yeye (Laizer) wanaogopa kuchangia hoja kutokana na tabia ya kuzomeana.
Aliwataka wajumbe kuwa wavumilivu ili
kuruhusu wajumbe kuchangia mijadala kwa uhuru.
na kuheshimiana kama ilivyotokea kwa baraza
la Wawakilishi Zanzibar ambako CCM ilikubali kugawa madaraka hata pale ambapo
hawakutaka kufanya hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BUNGE LIVUNJWE TUKAWA OMBE RADHI WANANCHI MJUMBE.”
Post a Comment