Monday, March 31, 2014
YANGA ,SIMBA AIBU YETU,AIBU YAO.
Do you like this story?
Azam imezidi kunyemelea
ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu baada ya kuichapa Simba 2-1, huku mabingwa
watetezi Yanga wakichapwa 2-1 na wachezaji 10 wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja
wa Mkwakwani, Tanga.
Mabao ya Hamisi Mcha na John Bocco yalitosha
kuipa Azam pointi tatu muhimu na kuongoza ligi kwa pointi 53, huku beki Joseph
Owino akifunga bao la kufutia machozi kwa Simba.
Nayo Mgambo wakicheza zaidi ya dakika 60
wakiwa pungufu waliwaduwaza Yanga kwa kuwachapa 2-1. Mgambo walikuwa pungufu
baada ya beki wao Mohamed Netto kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 30
na mwamuzi Alex Mahaji aliyehisi mchezaji huyo amevaa hirizi katika nguo yake
ya ndani, lakini alipokaguliwa haikuonekana. Mabao ya Mgambo yalifungwa na
Fully Maganga na Malima Busungu.
Wakati Yanga wakisuasusa na pointi 46, Mbeya
City imejiimarisha katika nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 45, baada ya
kuwafunga ndugu zao Prisons kwa bao 1-0.
Katika Uwanja wa Taifa; Mcha aliwainua
mashabiki wa Azam dakika ya 16 akiunganisha krosi kutoka upande wa kushoto
baada ya wachezaji wa Simba, Donald Musoti na Amis Tambwe kugongana walipokuwa
wakijaribu kumzuia Tchetche na kutoa mwanya kwa mfungaji kupiga shuti
lililomwacha kipa Mapunda asijue la kufanya.
Simba walisawazisha bao hilo dakika ya 45
baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na William Lucian kutua kichwani kwa Joseph
Owino na kuifungia Simba bao hivyo timu hizo kwenda mapumziko zikiwa 1-1 huku
mashabiki wa Yanga waliojitokeza uwanjani wakiishangilia Simba kwa nguvu.
Kipindi cha pili, Azam walimtoa Mcha na
kumwingiza Kelvin Friday dakika ya 52, mabadiliko yaliyokuwa na faida kubwa
kwao kwani dakika mbili baadaye Bocco aliifungia bao la pili akiunganisha mpira
uliopigwa na Tchetche na kugonga mwamba na kurudi uwanjani.
Mjini Tanga mshambuliaji Fully Maganga
aliifungia Mgambo Shooting bao la kuongoza dakika ya kwanza kwa kichwa
akiunganisha mpira uliokuwa umepigwa na kipa Juma Kaseja kwenda kwa Kelvin
Yondani.
Hata hivyo, katika mechi hiyo, Mgambo
walipata pigo baada ya Mohamed Netto kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 30 na
mwamuzi Alex Mahaji aliyehisi mchezaji huyo amevaa hirizi katika nguo yake ya
ndani, lakini haikuonekana.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub aliifungia
timu yake bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 51 baada ya beki
wa Mgambo, Novart Lufunga kumchezea vibaya mshambuliaji wa Yanga kwenye eneo la
hatari. Hii ni mara ya tatu kwa Yanga kushindwa kupata ushindi inapocheza dhidi
ya timu pungufu, walitoka 0-0 na Mtibwa na sare 1-1 na Azam. Busungu aliipatia
Mgambo bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 66 baada ya Kelvin Yondani kumwangusha
kwenye eneo la hatari.
Katika Uwanja wa Sokoine Mbeya
mshambuliaji Paul Nonga aliipatia Mbeya City bao la kuongoza dakika ya
pili baada ya kuwazidi mbio mabeki wote wa Prisons na kufunga bao hilo
lililoamsha shangwe.
Morogoro; Katika mchezo uliofanyika kwenye
Uwanja wa Manungu, wenyeji Mtibwa Sugar walienda mapumziko wakiwa mbele
kwa mabao 3-1, shukrani kwa mabao ya Jamal Mnyate dakika ya 14, Mussa
Hassan Mgosi (30), na Mohamed Mkopi (81), huku Behewa Behewa akiifungia Coastal
Union dakika ya 1
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “YANGA ,SIMBA AIBU YETU,AIBU YAO.”
Post a Comment