Monday, March 31, 2014

KIBADENI AJIGAMBA, ASEMA KUSHUKA NO.





 Kocha wa Ashanti United, Abdallah Kibadeni amesema atahakikisha timu yake inashinda mechi zake zilizobakia za Ligi Kuu ili wasishuke.

Kibadeni alisema hayo baada ya kuiongoza Ashanti kuichapa JKT Oljoro kwa mabao 2-0 juzi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yaliiwezesha Ashanti kufikisha pointi 21 na kukamata nafasi ya 11, huku wakiishusha Mgambo Shooting yenye pointi 19 mpaka katika nafasi ya 12.
Ashanti sasa ina mechi tatu mkononi dhidi ya Mbeya City itakayopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, Simba itakayoumana nayo Aprili 13 na Tanzania Prisons itakayopigwa Aprili 19 kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kibadeni alisema ushindi alioupata dhidi ya JKT Oljoro umeongezea morali kwa kikosi chake kutaka kufanya vizuri zaidi ili kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

“Hivi sasa hatuna muda wa kupoteza zaidi ya kuhakikisha tunashinda mechi mechi zote zilizobaki ili tucheze Ligi Kuu msimu ujao.
“Ni kazi ngumu kwa sababu mechi zote zilizobaki ni ngumu, lakini naamini kwa morali waliyonayo wachezaji wangu tutashinda,” alisema Kibadeni.

0 Responses to “KIBADENI AJIGAMBA, ASEMA KUSHUKA NO.”

Post a Comment

More to Read