Monday, March 31, 2014

JUMLA YA SHILINGI MILION 37,410,000 ZIMEPATIKANA KATIKA MECHI YA MBEYA CITY &TANZANIA PRISONS.


Kikosi cha Timu ya Mbeya City kikiwa katika mazoezi kabla ya Mechi na Tanzania Prisons

Timu ya Tanzania  Prisons ikiwa katika Mazoezi kabla ya Mechi.


JUMLA  ya shilingi milioni  37,410,000 zimepatikana katika mechi ya Mbeya City na Tanzania Prisons  iliyochezwa juzi katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine huku timu  ya Mbeya City ikiondoka na ushindi wa goli 1-0.

Akisoma mapato hayo Katibu  wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) Selemani Harubu , alisema kati mapato hayo shilingi milioni 8,467,499 zimeenda kwa kila timu.

Alisema, gharama ya Vat ni shilingi milioni  5,705610  tiketi shilingi 3,00,000 gharama ya mchezo 2,583,305huku  kamati ya ligi ikiondoka na shilingi 2,883,305.

Alisema,  TFF  imepata shilingi  1,291652 na MREFA ikiondoka na shilingi 1,004,618 na uwanja ukipata shilingi 4,305,508.

Aidha, baadhi ya viongozi wa timu za Tanzania Prisons na Mbeya City ambao hawakutaka kutajwa majina yao wameutaka  uongozi wa uwanja wa Sokoine kudhibiti mianya ya wazi ambayo imetokana na mashabiki kutoboa baadhi ya kuta na kuingia ndani ya uwanja.

0 Responses to “JUMLA YA SHILINGI MILION 37,410,000 ZIMEPATIKANA KATIKA MECHI YA MBEYA CITY &TANZANIA PRISONS.”

Post a Comment

More to Read