Monday, March 31, 2014
DKT. KIGODA:FANYENI KAZI KWA BIDII,MAARIFA NA UBUNIFU MKUBWA
Do you like this story?
![]() |
Waziri wa Viwanda na Biashara DktAbdallah Kigoda akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake unaofanyika JijiniDsm. |
![]() |
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizaraya Viwanda na Biashara ambao ni wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wanaoshiriki mkutano wao JijiniDsm |
Wafanyakazi wa Wizara
ya Viwanda na Biashara wametakiwa kuongeza juhudi na ubunifu katika utendaji wa
kazi ili kuiwezesha Wizara hiyo kufikia malengo yake iliyojiwekea.
Wito huo umetolewa na
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.DktAbdallah Kigoda, wakati akifungua Mkutano
wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwa siku mbili Jijini Dar
Es Salaam.
Dkt. Kigoda amesema,
Wizara ya Viwanda na Biashara ina jukumu kubwa katika kuboresha Uchumi wa Nchi
hivyo wafanyakazi hawana budi kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuiwezesha
Wizara kupata matokeo yaliyokusudiwa.
“Fanyeni kazi kwa
bidii, kwa maarifa na ubunifu mkubwa. Epukeni uzembe, ukiritimba usio na sababu
za msingi na zaidi ya yote, tujitangaze ili Umma ufahamu kikamilifu jitihada
zetu katika kukuza uchumi’’.
Awali akimkaribisha
Mh Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Uledi Mussa amesema, Uongozi wa Wizara
hiyo utaendelea kufanya jitihada za kuboresha maslahi ya wafanyakazi, mazingira
ya kufanyia kazi na kuondoa kero mbalimbali zinazowakwaza watumishi.
Kwa upande wake Mtoa
mada katika Mkutano huo Bi Honesta Ngolly ambae ni Afisa Elimu Kazi kutoka Tume
ya Usuluhishi na Uamuzi CMA, amewataka watumishi na Viongozi wa Wizara kutimiza
wajibu wao, kuheshimu sheria na miongozo ya kazi ili kuepusha migogoro katika
sehemu za kazi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DKT. KIGODA:FANYENI KAZI KWA BIDII,MAARIFA NA UBUNIFU MKUBWA ”
Post a Comment