Tuesday, March 18, 2014

DAKIKA TATU ZA WARIOBA MBELE YA MIMBARI YA BUNGE.




Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba, jaji joseph warioba jana jioni alisimama kwa dakika tatu mbele ya kipaza sauti lakini akashindwa  kuwasilisha rasimu ya katiba kutokana  na vurugu zilizojitokeza  bungeni.

Vurugu hizo zilitokea muda mfupi baada ya mwenyekiti wa bunge hilo Samuel sitta kumwalika kuwasilisha rasimu ya kativa kwa muda wa dakika 120.

Jaji warioba alisimama kwenye mimbari ya bunge saa 11:02 jioni tayari kuhutubia lakini kabla ya kufanya hivyo wajumbe kadhaa  walisimama na kuomba mwongozo wa mwenyekiti.

Waliosimama ni profesa Ibrahimu Lipumba, james mbatia,freeman mbowe, na tundu lisssu..

Hata hivyo sitta aliwanyima fursa akisema hakuna mwongozo hapa naomba mwenyekiti  uendelee , waheshimiwa wabunge  hakuna mwongozo naomba mwenyekiti uendelee kwa ajili ya hansard .

Kauli hiyo ilionekana kuchafua hali ya hewa kwani jaji warioba alipowasha  kipaza suti tayari  kuanza kuhutubia baadhi ya wajumbe walianza kupiga kelele  wengine makofi na kugonga  meza hivyo kumfanya ashindwe kufanya kazi hiyo ya uwasilishaji.

Waliokuwa mstari wa mbele kupinga jaji warioba  kuwasilisha rasimu ya katiba kwa sehemu kubwa walikuwa ni wajumbe wanaounda  kundi la umoja wa kativa ya wananchi(ukawa)

Jaji warioba akiwa anatafakari mble ya miambari sita aliwasha kpaza sauti  na kumtaka aendelee kuwasilisha rasimu ya katiba … endelea mwenyekiti  endelea kwa ajili ya kumbukumbu rasmi(hansard)

Lissu akisikika akijibu  kauli  hiyo akisema fuata kanuni mwenyekitu fuata kanuni  mwenyekiti  huku akipiga kelele na kugonga meza na wakati huo profesa lipumba akiwa amewasha kipaza sauti chake kutaka kuzungumza  huku naye akiendelea kupiga meza kwa nguvu.

Wengine waliosimama na mchungaji Christopher mtikila, Ezekiel oluoch, philimon ndesamburo, moses machali na mchungaji  peter msigwa.

Katika tatu zilikatika  huku kukiwa hakuna dalili za hali kutulia na kuona hivyojaji warioba aliamu kuondoka kwenye miambari na kuketi kimya akiwa na makamu mwenyekiti  wake jaji augustino ramadhani.

Baada ya hapo sitta alisimama na kuwasha kipaza sauti na kusema “waheshimiwa wajumbe katika mazingira  haya tuliyonayo naomba kutangaza  kuwa nasitisha shunguli za bunge hadi hapo tutakapo tangaziwa tena”

Licha ya kauli hiyo baadhi ya wajumbe waliendelea kupaza sauti zao  wakisema kwamba walikuwa wanaburuzwa.

Wakati hayo yakitokea kikoci cha askari wa bunge kiliingilia  ndani ya ukumbi na kusimama katika lango kuu hali iliyoonekana  kuwa ni kuchukua tahadhari  endapo hali ya usalama ingechafuka.

0 Responses to “DAKIKA TATU ZA WARIOBA MBELE YA MIMBARI YA BUNGE.”

Post a Comment

More to Read