Tuesday, March 18, 2014

GAVANA NDULLU: FEDHA ZA IPTL ZILIFUATA TARATIBU.




SAKATA la malipo ya kampuni ya kufua umeme ya independent  power Tanzania Ltd.(IPTL) limechukua sura mpya, baada  ya Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kuibuka na kuvunja ukimya na kusema haiwezekani  kuzuia wala kuhoji miamala  ya fedha za akaunti maalum ya Tegeta  Escrow  kwa sababu zilifuata taratibu zote za kisheria.

Katika ufafanuzi wake kwa waandishi wa habari jijini dare s salaam  jana Gavana wa Benki kuu Profesa Beno Ndullu amesema kuwa malipo hayo yalitolewa kihalali  na hakuna udanganyifu  wowote uliofanyika.

Amesema benki hiyo inawajibika kisheria  kutunza fedha hizo kutokana na makubalino ya kisheria  yaliyowekwa kati ya serikali  kupitia  wizara ya nishati na madini na kampuni ya IPTL mwaka 2006.

BOT ilitekeleza majukumu yake ya kulipa miamala  ya fedha kwa kampuni  ya kufua umeme ya  IPTL kwa sababu makubalino hayo yalifuata  taratibu za kisheria  kati ya serikali kupitia wizara ya nishati na madini na kampuni hiyo.

Katika ufafanuzi huo amesema kazi yao ni kuhakikisha wanatunza fedha hizo na kuzitoa kutokana na mkataba wa kisheria uliowekwa  baina ya wahusika  hao ambao ni serikali na IPTL yenyewe.

Kutokana na hali  hiyo BOT ilitekeleza makukumu yake ikijua kuwa jukumu la msingi na la asili  ni kulipa deni hilo pale inapotakiwa kufanya hivyo yaani  payment  on demand.

Amesema katika mazingira kama hayo demand ilifanyika pale wahusika  yaani serikali na IPTL walipotekeleza matakwa  ya kfungu cha 7.7 cha makubaliano  ya ufunguzi wa akaunti hiyo ya tegeta  Escrow.

Kwa hali hiyo mwaka 2013  wahusika hao wawili walisaini makubaliano ya kutoa fedha zilizomo katika akaunti hiyo ili zilipwe kwa IPTL jambo ambalo walilitekeleza.

0 Responses to “GAVANA NDULLU: FEDHA ZA IPTL ZILIFUATA TARATIBU.”

Post a Comment

More to Read