Tuesday, March 18, 2014

JK ABEBA SIRI NZITO BUNGE LA KATIBA.


 Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania


 Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuhutubia bunge maalumu la katiba ijumaa ya wiki  hii huku akitarajiwa  kuzungumzia masuala  mbalimbali  ikiwemo  mvutano uliojitokeza kuhusu namna ya kupiga kura na muundo wa serikali.

Akitoa tangazo hilo jana mwenyekiti wa bunge hilo Samuel sitta amesema Rais  ameona  ni busara kulihutubia  siku hiyo  kabla ya rais kuhutubia Bunge kuanzia  leo wajumbe watakuwa na semina ya siku nne kuhusu mambo mbalimbali  ikiwemo historia  ya muungano.

Kwa siku ya jumanne (Leo) kutakuwa na semini kuhusu kanuni zetu za bunge ambazo  zitatolewa ufafanuzi na wanasheria  wetu wa serikali na pia nitateua wajumbe wengine watatu kutoka katika kamati  ya kanuni kwa ajili ya kutoa ufafanuzi amesema.

Ameseme kesho na keshokutwa kutakuwepo na wajumbe watatu kutoka bara na watatu kutoka  Zanzibar wenye  uelewa kuhusu muungano ambao  watatoa  mada kuhusu historia  ya muungano.

Wajumbe hawa watatueleza historia ya muungano toka tulipotoka  hadi hapa tulipofikia  ili wajumbe wawe na uelewa mpana  kuhusu muungano , alisema sittta.

Aidha amesema ndani ya siku hizo pia wajumbe wawili  kutoka Kenya watatoa mada kuhusiana na uzoefu wao katika mchakato wa kutengeneza  katiba ambao nchi hiyo imeupitia.

Pamoja na bunge hilo kupitisha kanuni za bunge maalumu lakini wameshindwa  kupitisha vifungu vya 37 ana 38  ambavyo vinaelekeza namna ya kupiga kura katika kufanya maamuzi huku wajumbe wengi  kutoka vyama vya upinzani wakitaka ya siri na CCM   ikitakaya wazi.

0 Responses to “JK ABEBA SIRI NZITO BUNGE LA KATIBA.”

Post a Comment

More to Read