Tuesday, March 18, 2014

UKAWA WAELEZA SABABU ZA KUMZUIA WARIOBA.




Mwenyekiti wa Bunge maalumu la katiba Samuel sitta alipata jaribuo la kwanza baada ya baadhi ya wajumbe kupinga kuruhusiwa kwa mwenyekiti  wa tume ya mabadiliko ya katiba jaji Joseph Warioba  kuwasilisha rasimu ya katiba kwa madai ya ukikwaji wa kanuni za bunge.

Wajumbe hao chini ya umoja wa katiba ya watanzania(ukawa) walitangaza mapema jana kwamba wangepinga ratiba nzima kuendlea hadi madai yao ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete  afungue bunge . kwanza kabla ya rasimu kuwasilishwa yasikilizwe.


Katika uamuzi huo ulifikiwa jana mchana mmoja wa viongozi wa ukawa profesa ibrahimu lipumba amesema kwa sababau  za ukikwaji wa kanini tuapenda  kueleza kwamba hatupo tayari kuunga mkono  tutapinga  kwa kadri uwezo wetu mambo makubwa manne kufanyika bungeni.

Amesema mambo ambayo wanapanga ni uwasilishaji wa rasimu ya kativa uliopangwa kufanyika jana kabla ya ufunguzi  wa bunge  maalumu unotarajiwa  kufanywa na Rais Kikwete.

Profesa lipumba pia alisema wangepinga kufanyika kwa semina ambyo ilipangwa kuongozwa  na wataalamu wa ndani au nje ya nchi leo kuhusu uzoefu katika masuala ya bunge la katiba.

Pia tutapinga hotuba ya Rais endapo itatolewa baada ya uwasilishaji  wa rasimu ya katiba na pia jambo jingine lolote linalokiuka kanuni za bunge maalumu amesema profesa lipumba aliyeambatana na wajumbe wenzake james mbatia na tundu lissu.

0 Responses to “UKAWA WAELEZA SABABU ZA KUMZUIA WARIOBA.”

Post a Comment

More to Read