Monday, March 31, 2014
DARAJA LA RUVU LAFUNGWA, MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AWAPIGA 'STOP' WAKAZI WA KIWANGWA KWENDA BAGAMOYO.
Do you like this story?
![]() |
Vijana hao waliwavusha hadi wagonjwa katika eneo hilo kama anavyoonekana pichani akiwa amembeba mtu mzima anayeonekana kuwa ni mgonjwa. |
![]() |
Vijana wakijipigia debe kwa dereva ili akibali kuvushwa, bila kujua kuwa ndani yake alikuwapo Mkuu wa Wilaya hiyo. |
Wakazi wa Kiwangwa, wa Kiwangwa, wakivushwa na
vijana waliojitolea kujipatia ajila katika Daraja la Ruvu kwa kuwavusha
wananchi kwa kuwabea ama kuwaongoza njia ili kuvuka eneo hilo la daraja
lililojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Kamera ya
Sufianimafoto iliwashuhudia viajana hao wakiwavuja raia katika eneo hilo kwa
ujila wa Sh. 2000 kwa kila aliyebebwa mgongoni asiyetaka kuvua viatu ama kugusa
maji hayo, na Sh. 500 kwa kushikwa mkono kuongozwa njia kutoka mwanzo wa maji
hayo hadi kuyavuka, na kuyaongoza magari kuvuka eneo hilo ni Sh. 3000 hadi
5000.
Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana, Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alifika eneo hilo na kujionea wananchi
wakitaabika kuvuka ene hilo na huku magari ya abiria yaliyokuwa yakitokea
Bagamoyo kwenda Kiwangwa, yakibeba abiria na kuishia eneo hilo na kubeba
wengine walioshushwa upande wa pili na kugeuza kwa kila abiria kulipa Sh. 1000.
Na kisha abiria hao wakipata usafiri mwingine wa kubebwa na Vijana waliopo eneo
hilo kwa Sh. 2000 kwa aliyependa ama 500 kwa kuongozwa njia.
kuamua kuagiza askari Polisi wenye silaha ili
kulinda eneo hilo kuwazuia waanchi kuvuka ili kuepuka maafa.
Baada ya hapo Mkuu huyo wa Wilaya aliwatoa
tamko na kuwataka wakazi wa Kiwangwa kutokwenda Bagamoyo na waBagamoyo
kutokwenda Kiwangwa, kwa kipindi chote cha mvua ili kuepuka maafa yanayoweza
kutokea kwa kutumbukia na kusombwa na maji, ama daraja hilo la Jeshi kukatika
kutokana na maji kuanza kupita juu ya daraja hilo jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DARAJA LA RUVU LAFUNGWA, MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AWAPIGA 'STOP' WAKAZI WA KIWANGWA KWENDA BAGAMOYO.”
Post a Comment